Thursday, February 16, 2017
KUTOKA CENTRAL POLISI KAMANDA SIRRO ANAZUNGUMZA
#DawaZaKulevya
'Jumla ya watuhumiwa 16 wamepelekwa mahakamani na majalada yao 24 yapo kwa wakili wa serikali kwa ajili ya uchunguzi.' Sirro
-Watuhumiwa 16 akiwemo Agnes Masongange kesho watapelekwa kwa mkemia mkuu kwa uchunguzi,na ikabainika wanatumia sheria itachukuliwa dhidi yao
-'Tumekamata jumla ya kete 612 za madawa ya kulevya aina ya heroine,puli za bangi 816,misokoto ya bangi 89 na bunda 19 za mirungi..'
-Operesheni ya ukamataji wanaojihusisha na Dawa za Kulevya inaendelea. Jumla ya watuhumiwa 349 wamekamatwa, operesheni ilioyoanza trh 1 Feb. - Kamanda Sirro
-'Watuhumiwa 9 ambao ni Askari polisi wamekabidhiwa kwa Kamishna wa Kupambana na Madawa ya kulevya kwa uchunguzi.'
Akizungumza leo Jijini Dar es Salaam, Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, Kamishna Simon Sirro amesema kati ya watuhumiwa hao, wamo wauzaji, wasafirishaji na watumiaji wa dawa za kulevya, na kwamba wataanza kufikishwa mahakamani siku ya kesho, huku mmoja akipandishwa kizimbani leo.
Pia ametoa taarifa ya kijana mmoja anayedaiwa kusambaza taarifa za uongo, ambapo amesema kuwa jeshi hilo linamshikilia kijana huyo ambaye ni mwanafunzi mwenye umri wa miaka 23, anayedaiwa kutaja majina ya viongozi na kuwatuhumu kuwa wanahusika na dawa na dawa za kulevya.
Kuhusu askari 9 waliotuhumiwa kuhusika na dawa hizo, Kamanda Sirro amesema askari hao wamekabidhiwa kwa Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya kuzuia na Kupambana na Dawa za Kulevya kwa ajili ya kuchukuliwa hatua za kisheria.
Kamanda Sirro amesema hadi sasa jumla ya kete 612 pamoja na bangi vimekamatwa na kwamba kuna watu wengine 17 ambao bado jeshi hilo linawafuatilia na watakuwa mbaroni wakati wowote.

Monday, February 13, 2017
NJAA & UKAME=KIFO
Wakati Watanzania wakiwa wameelekeza hisia zao katika mapambano dhidi ya madawa ya Kulevya kuna matatizo kadhaa ambayo yamewekwa pembeni na kuacha kujadiliwa na kushughulikiwa.
Wakati Watanzania wakiwa wameelekeza hisia zao katika mapambano dhidi ya madawa ya Kulevya kuna matatizo kadhaa ambayo yamewekwa pembeni na kuacha kujadiliwa na kushughulikiwa.
Mojawapo ya masuala hayo ni Njaa ambayo katika kipindi cha miezi kadhaa imebainika kwamba kuna tatizo kubwa la ukosefu wa chakula katika nchi hiyo ya Afrika Mashariki kutokana na ukame uliolikumba eneo zima la ukanda huo ikiwa ni pamoja na Kenya, Uganda na Somalia.
NI KWELI MAKONDA ANAWEZA KUMFUKUZA MTU DAR ES SALAAM
Na: Tundu Lissu
Kauli ya leo ya Mkuu wa Mkoa wa Dar Paul Makonda kwamba ana uwezo wa kumhamisha mtu yeyote kutoka kwenye Mkoa wake ni mfano mwingine wa aina ya wanasiasa waliopewa madaraka na Rais Magufuli ambayo hata hawayaelewi na, kwa sababu hiyo, hata wao wenyewe hawajielewi.
Nafasi ya Wakuu wa Mikoa imetambuliwa na ibara ya 61 ya Katiba yetu. Ibara ya 61(4) inafafanua kwamba kila Mkuu wa Mkoa atatekeleza kazi na majukumu yaliyofafanuliwa na, au chini ya, sheria yoyote iliyotungwa na Bunge.
Sheria iliyotungwa na Bunge kwa ajili ya kufafanua kazi na majukumu ya Wakuu wa Mikoa ni Sheria ya Tawala za Mikoa ya 1997.
Sheria hiyo ndiyo iliyowapa Wakuu wa Mikoa na Wilaya mamlaka ya kipolisi, yaani mamlaka ya kukamata watu wanaosadikiwa kufanya makosa ya jinai mahali ambapo hakuna askari polisi.
Mamlaka haya ni madogo sana tofauti na Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina ya Makonda wanavyoamini au kuaminishwa.
Kwanza, ni mamlaka ya nyongeza (supplementary powers) tu kwa mamlaka ya Jeshi la Polisi ambalo ndilo lenye mamlaka hasa ya kukamata wahalifu.
Hii ina maana kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya hawezi kutumia mamlaka ya kipolisi pale ambapo tayari kuna askari polisi. Polisi wanatakiwa wafanye kazi yao bila kuamriwa na Mkuu wa Mkoa au Wilaya.
Pili, mamlaka ya kipolisi yamewekewa masharti ya muda, yaani, mtu aliyekamatwa kwa amri ya Mkuu wa Mkoa au Wilaya anatakiwa apelekwe mahakamani au aachiliwe huru ndani ya muda wa masaa 48.
Tatu, Mkuu wa Mkoa au Wilaya aliyetoa amri ya kukamata mtu chini ya mamlaka yake ya kipolisi, anatakiwa - haraka iwezekanavyo - kupeleka taarifa ya maandishi kwa hakimu juu ya kukamatwa kwa mtu huyo na sababu zake.
Sheria imeweka wazi kwamba Mkuu wa Mkoa au Wilaya asiyetekeleza masharti haya hataruhusiwa kumkamata mtu huyo kwa kosa hilo hilo na anaweza kushtakiwa mahakamani kwa kosa la matumizi mabaya ya madaraka yake.
Hakuna mahali popote katika Sheria ya Tawala za Mikoa ambako Mkuu wa Mkoa au Wilaya amepewa mamlaka ya kumwondoa mtu yeyote kwenye Mkoa au Wilaya yake.
Mamlaka ya kuondoa watu kwenye maeneo yao, yaani deportation, yalikuwa sehemu ya mamlaka ya Rais kwa mujibu wa Sheria ya Kuondoa Watu (Deportation Ordinance).
Sheria hii ya kikoloni ilitangazwa kuwa kinyume na Katiba, na kwa hiyo batili, na Jaji James Mwalusanya wa Mahakama Kuu katika kesi maarufu ya Chumchua Marwa na Wenzake ya mwaka 1987.

Ni wazi Mkuu wa Mkoa wa aina ya Paul Makonda hawezi kufahamu mambo makubwa kama haya. Kwake yeye na kwa Wakuu wa Mikoa au Wilaya wa aina yake, kuwa Mkuu wa Wilaya au Mkoa ni sawa na kuwa Rais wa Mkoa au Wilaya aliyokabidhiwa.
Wakuu wa aina hii wanahitaji kuelimishwa kwamba wao hawana mamlaka ya kifalme aliyo nayo Magufuli.
Na namna bora kabisa ya kuwaelimisha ni kuwashtaki kwa madai mahakamani pale wanapoenda nje ya masharti ya madaraka yao. Tutaanza na Paul Makonda.

![]() |
Bw. Poul Makonda |
Sunday, February 12, 2017
JECHA AMEIFISIDI AKILI YAKE
Na Jabir IdrissaNILIPATA kusema kuwa Jecha Salim Jecha amejidhalilisha, amejidharau na kujishusha hadhi. Haaminiki tena pamoja na kuwa ni mstaafu kiutumishi.
Alistaafu utumishi serikalini kwa mujibu wa sheria, akiwa ametimiza umri wa miaka 60 miaka kadhaa iliyopita, lakini amejiingiza katika kusema asichokiamini.
Haoni aibu wala tatizo kudanganya. Alizuga kwa staili ya kujitia hamnazo siku ile ya 28 Oktoba 2015, alipotoa tangazo la kufuta uchaguzi mkuu wa Zanzibar, akiwa chini ya ulinzi wa dola ilhali alijua hakuwa na mamlaka ya kisheria ya alichokifanya. Wala hakujali kama alijishusha na hajasafika.
Bado anaendelea kuzuga watu hata leo, katika jitihada zake dhaifu za kutetea upuuzi ule ulioelekeza kuilazimisha nchi kuingia kwenye balaa la damu; mwenyewe akidai ndio alikuwa anaiokoa nchi na balaa.
Alifuta uchaguzi wakati alikuwa na uhakika kwamba anadhulumu wananchi haki yao ya kuchagua na hivyo kuamua kwa hiari yao kuongozwa na mtu mwingine asiyekuwa kipenzi chake Dk. Ali Mohamed Shein, anayetoka Chama Cha Mapinduzi (CCM).
Jecha alijua hakuna sheria inayohalalisha mtu yeyote au hata hiyo tume anayoiongoza kuufuta uchaguzi ambao tayari umeshafanyika. Alijua hilo, ndio maana alitolea tangazo mafichoni akiwa ametelekeza tume na makamishna wake.
Asiyetulia akili sawasawa kama yeye, anakubaliana naye kuwa uamuzi wa kufuta uchaguzi mkuu uliokuwa huru, wa haki na ambao ulionesha uhalisia wa maamuzi ya wananchi wa Zanzibar – kama vile yeye mwenyewe alivyothibitisha kupitia taarifa yake kwa vyombo vya habari siku ya 26 Oktoba 2015 – uliepusha balaa.
Eti uliepusha balaa kwa sababu Zanzibar haikuingia kwenye machafuko. Kwamba kwa akili yake na hao wenzake, Zanzibar ni tulivu, kwa kuona watu wanaendelea na shughuli zao. Huko ni kuzuga kwa kiwango cha juu.
Andika maneno “uchaguzi mkuu Zanzibar 2015” kwenye zana ya kupekulia taarifa mtandaoni leo, uone kitakachokuja haraka. Nimekuta taarifa ya Tume ya Uchaguzi Zanzibar (ZEC) ya matokeo ya uchaguzi wa rais ambayo yamehakikiwa kutoka baadhi ya maeneo ya Zanzibar.
Majira ya saa 2 usiku, tarehe 27 Oktoba 2015, tume ilikuwa imeshatangaza matokeo ya majimbo 31 kati ya 54 yote yaliyokuwa na idadi ya wapigakura 503,860 walioandikishwa na kuingizwa kwenye Daftari la Kudumu la Wapigakura la Zanzibar.
Matokeo ya kura za urais yaliyokuwa yametangazwa kufikia muda huo yalionesha:
Jina Chama Kura Asilimia
Khamis Iddi Lila ACT-W 189 0.1
Juma Ali Khatib ADA-TADEA 93 0.0
Hamad Rashid Mohamed ADC 252 0.1
Said Soud Said AFP 223 0.1
Ali Khatib Ali CCK 240 0.1
Ali Mohamed Shein CCM 139,557 57.9
Mohammed Masoud RashidCHAUMMA 257. 0.1
Seif Shariff Hamad CUF 93,699 38.9
Taibu Mussa Juma DM 118 0.0
Abdalla Kombo Khamis DP 86 0.0
Kassim Bakar Ally JAHAZI 227 0.1
Seif Ali Iddi NRA 63 0.0
Issa Mohammed Zonga SAU 127 0.1
Hafidh Hassan Suleiman TLP 107 0.0
Leo, Jecha anapomuita Maalim Seif Shariff Hamad kuwa ni muongo na mtu aliyetangaza matokeo ya uchaguzi yasiyokuwepo popote duniani, anamaana gani kama sio kuzuga? Ila ajue anazuga tu wasiojua na wale wasiofikiri kwa akili zao kama alivyo.
Hata mara moja hawezi kudanganya wale wanaojua, wakiwemo mawakala walioshiriki kazi ya kuhesabu na kuzihakiki kura za urais vituoni. Hakukuwa na kura nyingine zaidi ya hizo zilizosimamiwa na tume anayoongoza na kuidhinishwa na watendaji iliowaajiri kazi.
Jecha hajafaulu kuwazuga watazamaji wa uchaguzi wa ndani ya jamhuri na wale waliotoka asasi za mataifa mengine. Hadanganyi hata watazamaji wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC) wala wa Jumuiya ya Ushirikiano ya Kusini mwa Afrika (SADC), ambao wananyamaza tu kwa kuwa hawana uamuzi wa kijasiri.
Kwamba Maalim Seif ni muongo, Jecha anakusema leo ikiwa ni zaidi ya mwaka mmoja tangu alipothibitisha roho yake ilivyo mbaya kwa kiongozi huyo mstaarabu, mtaalamu wa siasa, mwalimu na mtu mwenye mapenzi mema na nchi.
Pemba, kule ambako Jecha bila ya aibu anadai uchaguzi uliharibika, kazi ya kuhesabu na kuhakiki kura za urais ilifanywa kwa uangalifu kama sheria inavyotaka. Waliosimamia ni watendaji wa tume ambao hatimaye walituma matokeo makao makuu ya tume bila kusita.
Tatizo ni pale Jecha ambaye amethibitisha alikuwa akihangaika kuhakikisha anatimiza matakwa ya CCM, alipokuta zaidi ya asilimia 90 ya kura za kisiwani Pemba zilimkataa kipenzi chake.
Hapo ndipo mahangaiko yakaanza. Jitihada za kubadilisha matokeo zilikwama kwani hesabu yote ilikuwa tayari mikononi mwa Maalim Seif kupitia watendaji wake. Hata mbinu za kimafiya za kutaka kutumia mawakala wa CUF ili wapitishe matokeo yaliyopikwa, zilishindwa.
Huyu Jecha amebadilika sana kiutu kwa kweli kiasi cha kustahili kuonewa huruma. Pengine ikielezwa asijifiche na hataguswa, labda atarudi kwenye akili zake ambazo amezifisidi mwenyewe. Ajabu, ni nani ametangaza kumdhuru? Hofu yake na aliowatumikia.
Huku akijua fika kuwa anaishi kwenye makwapa ya dola inayomlinda kwa sababu ya uovu huo wa dhulma alioshiriki kuutenda, amekuja na kioja hicho kupitia mahojiano aliyoruhusiwa kufanya na aliowafurahisha, na kwa sababu wana ‘maguvu’ ya maamuzi.
Jecha alisafiri kwenda Dar es Salaam na kufanya mahojiano na Tido Mhando, mtangazaji maarufu nchini na naibu mkurugenzi wa kituo cha televisheni cha Azam (Azam Tv) kupitia kipindi cha Funguka kinachorushwa kila Jumapili kuanzia saa 3 asubuhi.
Ni katika mahojiano hayo alitoa maelezo ya kuzuga watu. Eti kwamba jazba za kisiasa ndio tatizo la Zanzibar. Kwa hivyo naye alikumbwa na jazba hizo alipotakiwa kueleza huo uharibikaji wa uchaguzi ulikuwa maeneo gani wakati haukuripotiwa kwa muda wote watu wakipiga kura mpaka vituo vilipofungwa?
Kazi ya kuhesabu kura, kuzihakiki na hatimaye kuidhinisha matokeo kutangazwa ilikamilika ndio maana yeye mwenyewe alishuhudiwa akitangaza matokeo ya majimbo yale 31.
Hivi ingekuwa mgombea wa CCM alishinda kura halali, Jecha angethubutu kukimbia kazi ya kusimamia kutangaza matokeo yaliyobakia baada ya hayo 31 kuyatangaza hadharani?
Au je, Jecha angeufuta uchaguzi kama alikuwa na uhakika mgombea kipenzi chake, Dk. Shein, alikuwa na kura kisiwani Pemba za kuendeleza ushindi wa kura za Unguja zilizokwishampatia karibu kura 140,000 (asilimia 57)?
Akili ya kawaida inathibitisha alijiachia kwa raha zake, akajipeleka mikononi mwa watawala waovu na wang’ang’anizi wa madaraka, badala ya kukamilisha kazi aliyoteuliwa kuifanya, na kusoma takwimu ambazo yumkini hata sasa haziamini.
Ukweli huu wa Jecha kuhujumu haki baada ya kifisidi akili zake, utaendelea kumzonga kifuani kadiri anavyojitahidi kuzuga watu. Utamdhoofisha tu kama wanavyoumia walionufaika na hujuma aliyoitenda.
Thursday, February 9, 2017
wafuasi wa Gwajima wafurika kituo kiukuu cha polisi
Wafuasi na waumini wa kanisa la ufufuo na Uzima wamemiminika maelefu kwa mamia wanaimba na kusifu mbele ya kituo kikuu cha polisi Dar ambao kiongo wa kiroho wa kanisa hilo Mh Gwajima anahojiwa kwa madai ya kujihusisha na biashara ya madawa ya kulevya.
![]() |
wafasi wa Mchungaji Joephati Gwajima wakiwa katika viwanja vya polisi |
Watu 13 wauawa kwenye shambulizi la kujitoa muhanga Afghanistan
Shambulizi la kujitoa muhanga dhidi ya mahakama Kuu ya Afghanistan, lililotokea jana mjini Kabul limesababisha vifo vya watu 13 na wengine 25 kujeruhiwa.
Shambulizi hilo lilitokea jioni wakati wafanyakazi walipokuwa wakitoka kazini, ni la pili dhidi ya mahakama hiyo katika muda wa miaka mitatu. Hadi sasa hakuna kundi lililotangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Wizara ya afya ya Afghanistan imethibitisha kutokea kwa vifo hivyo, na kusema watu 41 waliojeruhiwa wamepelekwa hospitali. Lakini mashuhuda wamesema idadi ya vifo na majerahi ni kubwa kuliko iliyotangazwa.
Umoja wa Mataifa umelaani vikali shambulizi hilo na kutoa rambirambi kwa familia za wahanga na kwa serikali ya Afghanistan.

Tuesday, February 7, 2017
MJUE KAMANDA #VALENTINE_STRASSER
..KUTOKA URAIS HADI OMBAOMBA MTAANI.
Duniani Tunajifunza na kuona vitu vingi tofauti vya kushangaza, kuogofya na kufurahisha. Wengi hawamjui Valentine Strasser ambaye aliwahi kuwa rais wa nchi ya Sierra Leone kati ya Aprili 29, 1992 hadi Januari 16 , 1996 akiwa ndiye amiri jeshi mkuu na kiongozi wa ngazi ya juu kwenye taifa hilo lililopo kaskazini-magharibi mwa bara la Afrika.Wakati akiingia madarakani aliweka rekodi ya kuwa kiongozi mwenye umri mdogo zaidi, yaani akiwa na chini ya miaka 25.Kapteni Valentine Strasser kiongozi wa mapinduzi ya Rais Saidu Momoh.Aprili 29, 1992, Strasser akiwa kijana mwanajeshi mwenye cheo cha kapteni, akiwa na umri wa miaka 25, aliwaongoza wanajeshi wenzake kuvamia Ikulu ya Sierra Leone, walimkuta rais amejificha ndani ya kabati lililopo kwenye chumba cha kuogea, kisha wakamteka Rais Joseph Saidu Momoh na wakamlazimisha kukimbia, naye akatorokea Conakry, Guinea.
Valentine Strasser baada ya mapinduzi kufanikiwa.
Strasser alichukua madaraka ya nchi hiyo siku tatu tangu ashehereke sikukuu yake ya kuzaliwa.
Baada ya Momoh kutorokea Conakry, Strasser alijitangaza kuwa Rais wa Sierra Leone. Aliwaongoza vijana wenzake sita waliofanikisha mapinduzi hayo na kuunda serikali ya mpito waliyoipa jina la National Provisional Ruling Council (NPRC).
Maisha yakabadilika, alishakuwa mkuu wa nchi, kwa hiyo hakutaka kuishi kwenye nyoyo za Wasierra Leone.
Hakulipa malimbikizo ya mishahara ya wanajeshi na watumishi wengine wa umma.
Alifuja almasi ya Sierra Leone, kwa vile jina lake ni Valentine, basi sikukuu ya Valentine’s Day akaifanya kuwa sherehe ya kitaifa yenye mapumziko huku sherehe kubwa ikiandaliwa ikulu ya nchi hiyo.
Strasser alikuwa na mbwembwe nyingi, mwaka 1993 katika mkutano wa wakuu wa serikali katika nchi za Jumuiya ya Madola, uliofanyika Limassol, Cyprus, alitinga kwa mbwembwe akiwa amevaa suruali ya jeans na fulana yenye maandishi Sunny Days in Cyprus (Siku za Jua Kali Cyprus).
Alikuwa mtu wa starehe, vurugu nyingi kwa wanawake, aliua watu wasio na hatia.
Strasser alisahau kuwa ipo siku uongozi hautakuwa kwenye mikono yake, na ambacho kinaweza kumfaa ni kuishi ndani ya mioyo ya watu ili wamtetee na kumpigania baadaye. Januari 16, 1996, Strasser alipinduliwa na msaidizi wake, Brigedia Jenerali Julius Maada Bio.
Strasser akakimbilia Uingereza, akajiunga na Chuo Kikuu cha Warwick, kilichopo mjini Coventry, akaanza masomo ya sheria, akasema anataka awe wakili ili awatetee Waafrika.
Mwaka mmoja wa masomo, Strasser aliishiwa fedha, akaacha chuo.
Maisha Uingereza yakawa magumu, akakimbilia Gambia nako kukawa pagumu, mwisho akarudi Sierra Leone, mjini Grafton, mashariki mwa mji mkuu wa nchi hiyo, Freetown. Kazi ya kwanza ambayo Strasser aliifanya, ikawa kuanzisha kichuo kidogo cha kufundisha kompyuta na teknolojia ya habari na mawasiliano (Tehama). Maisha ya chuo yakamshinda.
Baada ya kila kitu kwenda kombo, Strasser alirudi nyumbani kwa mama yake mzazi na kuishi kwenye banda la uani. Hata sasa, akiwa na umri wa miaka 49, anakunywa pombe za kienyeji mtaani.
Picha ya Valentine Strasser alivyo sasa.
Hana hadhi yoyote kama kiongozi mkuu wa nchi mstaafu. Strasser anaishi kama mtu wa kawaida tu mtaani. Mlevi na hakuna anayemjali.
Hana mtu wa kumtetea wala kumpigania kwa sababu hakuishi kwenye nyoyo za watu. Strasser ndiye mkuu wa nchi wa zamani, anayeishi kimaskini kuliko wakuu wote wa nchi duniani.
Ukiwa kiongozi na kugeuka kituko kama Strasser inawezekana kabisa.
Ishi vibaya na watu wasikupende, akija mtawala ambaye hatakutambua kama mkuu uliyepita, unaweza kuishi maisha ya hovyo kama ombaomba mtaani au kuwa mnywa gongo uliyeshindikana.
Vyema sasa viongozi wote duniani watambue kwamba uongozi ni dhamana, wafanye kazi kwa kujituma na wataishi mioyoni mwa wananchi waliowaongoza milele. Kuna viongozi wengi waliofanya mema na bado wanaenziwa mpaka sasa kama Julius Nyerere na Nelson Mandela, wako wengi hawa ni baadhi tu ya viongozi walioweka mbele maslahi ya wananchi wao na watakumbukwa milele.
Subscribe to:
Posts (Atom)