Waziri Nchemba: Maiti Saba wa Mto Ruvu ni wahamiaji haramu
Mheshimiwa Mwigulu NCHEMBA (wewe ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi)..,
.., leo asubuhi ulikuwa katika kipindi cha Tuongee Asubuhi
kinachorushwa na kituo cha matangazo cha Star TV.., nimekusikia kauli
zako, kuhusu 'issue' ya watu wale 7 waliokutwa mto Ruvu wakiwa wamekufa
(vifo vya ajabu), umesema kwamba watu wale ni WAHAMIAJI HARAMU .., mimi
nikuulize maswali yafuatayo;
(i) Je, wahamiaji haramu ndiyo wanapaswa kuuwawa na kutupwa mto Ruvu!?
(ii) wahamiaji haramu ndiyo wanapaswa kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali na kuuawa!?
(iii) wahamiaji haramu ndiyo wanatakiwa kuuwawa na kufungwa kwenye mifuko ya Sandarusi na kuwekwa mawe ndani!?
(iv) sheria za nchi, sheria za jeshi la polisi, sheria za idara ya uhamiaji zinasema nini kuhusu wahamiaji haramu.., kuuwawa!?
(v) kama kweli ni wahamiaji haramu.., nani ametoa idhini ya kuwaua,
nani amewaua, na kwanini watupwe mto Ruvu wakiwa wamefungwa kwenye
mifuko na mawe ndani yake!?
.., niendelee kukuliza mheshimiwa
waziri.., hao wahamiaji haramu, wanatoka katika nchi gani.., Je, nchi
zao zikigundua kwamba mliwaua watu wao na kuwazika huko Bagamoyo, hauoni
mnaleta mgogoro mkubwa wa kidiplomasia!?
Mheshimiwa waziri, kazi
ya jeshi la polisi ni kulinda watu na mali zao, kuhakikisha usalama wa
raia ni kiwango cha juu, bila kuhatarisha usalama wao, maana wao ndiyo
kipaumbele cha kwanza cha serikali (walipa kodi)..,
.., umetoa
ufafanuzi hafifu sana kuhusu suala la kupotea kwa Ben Saanane na
kutoonekana kwa kitambo kirefu.., kuna maswali ya kuoanisha hapa;
(i) kwanini ile miili 7 iliyokutwa kule Ruvu izikwe kwa haraka ile na halmashauri!?
(ii) kwanini jeshi la polisi, halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo hawakutaka kufanya uchunguzi kubaini nini chanzo!?
(iii) kwanini jeshi la polisi liko kimya hadi sasa, wiki nzima, hadi
'pressure' ya watanzania inakuibua wewe waziri, tena kwa kuulizwa!?
(iv) Je, wakati huu ndugu, jamaa, rafiki wa Ben Saanane wakiwa katika
sintofahamu ya ndugu yao, kwanini Jeshi la polisi halikuona umuhimu wa
kutokuzika maiti zile kwa haraka ile!?
(v) kuna kila sababu ya
kumtaka OCD wa Bagamoyo na vyombo vya ulinzi na usalama katika
halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, kutoa kauli yenye kueleweka.., (wako
chini ya ofisi yako hawa watu)
NB; Pia.., kuna habari moja iliwahi kutangazwa na ITV mwezi wa August, mwaka 2016, naomba kunukuu sehemu ya habari ile..,
".., Zaidi ya watanzania 56 katika vijiji vya Chamchuzi na Buguluka
vilivyoko katika kata ya Bwelanyange iliyoko wilayani Karagwe mkoani
Kagera waliokuwa wakijihusisha na shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera
na ziwa hiema wanadaiwa kutekwa na kuuawa kikatili na watu wanaodhaniwa
kuwa ni askari wa nchi jirani Rwanda ambao mara kwa mara hufanya doria
ndani ya mto huo na ziwa hilo. "
.., kitu cha kusikitisha sana..,
serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi.., haikuwahi kutoa
kauli, taarifa yoyote juu ya habari hiyo.., mbaya sana!
Mwisho ;
Jeshi la polisi kupitia intelejensia yake, wanapaswa kuwa 'proactive'
kuliko kuwa 'reactive' kwenye masuala ya ulinzi wa mali za umma na
usalama wa raia.., intelejensia ya jeshi la polisi inatakiwa kufanya
kazi kubwa kabla umma kupiga kelele ndiyo wao wachukue hatua.., (kama
jeshi la polisi linaweza kubaini kuhusu vurugu kutokea katika mkutano wa
kisiasa ambao haujafanyika.., linashindwa nini kubaini usalama wa raia
na mali zao!?)
matukio ya watanzania kuuwawa yamekuwa
yakiongezeka kila kunapokucha, watanzania 9 katika wilaya ya Kyelwa
waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera waliuwawa na
watu wanaodhaniwa askari wa nchi jirani ya Rwanda hali ambayo
ilikusikitisha wewe (waziriwa mambo ya ndani) wakati huo ukiwa katika
ziara ya kikazi katika mkoa wa Kagera.., (lakini wizara yako haikutaka
kutoka mbele ya watanzania na kusema kitu, kuhusu matukio hayo)
Jeshi la polisi linapawa kuwa jeshi la kulinda raia na mali zao.., siyo
jeshi la kulinda maslahi ya watu wachache sana katika Jamhuri ya
muungano wa Tanzania.., tazama, raia wanakufa vifo vya ajabu katika nchi
yao, zinatoka kauli rahisi, kwamba ni wahamiaji haramu.., siyo
sahihi.., tunapaswa kupata ukweli dhidi ya maiti zile zilzokutwa katika
mto Ruvu.., pia tuelezwe;
(i) kwanini zitupwe mto Ruvu.
(ii) kwanini zifungwe na mawe ndani.
(iii) kwanini zifungwe katika mifuko ya Sandarusi.
(iv) kwanini zionekane kujeruhiwa na vitu vyenye ncha kali.
(v) kwanini mamlaka za usalama ziko kimya..,
Ahsante,
Mwananchi wa kawaida,
Martin Maranja Masese (MMM)
Source JF
 |
waziri wa mabo ya ndani Ndg Mwigulu Nchemba |