Watoto elfu 17 waandikishwa kama askari watoto kwenye mgogoro nchini Sudan Kusini
Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, tangu mgogoro wa kijeshi ulipotokea nchini Sudan Kusini miaka mitatu iliyopita, watoto elfu 17 wameandikishwa kwenye makundi ya wapinzani askari watoto.Takwimu zilizotolewa na shirika hilo zimeonyesha kuwa, mpaka sasa ni askari watoto 1,932 tu wameachiwa huru.
Kuanzia mwaka huu, Shirika hilo na mashirika mengine yamepokea watoto laki 1.8 wanaokabiliwa na utapiamlo, na idadi hii imeongezeka kwa asilimia 50 kuliko mwaka jana.
No comments:
Post a Comment