Friday, December 16, 2016

Watoto elfu 17 waandikishwa kama askari watoto kwenye mgogoro nchini Sudan Kusini

Shirika la Kuhudumia Watoto la Umoja wa Mataifa UNICEF limesema, tangu mgogoro wa kijeshi ulipotokea nchini Sudan Kusini miaka mitatu iliyopita, watoto elfu 17 wameandikishwa kwenye makundi ya wapinzani askari watoto.

Takwimu zilizotolewa na shirika hilo zimeonyesha kuwa, mpaka sasa ni askari watoto 1,932 tu wameachiwa huru.

Kuanzia mwaka huu, Shirika hilo na mashirika mengine yamepokea watoto laki 1.8 wanaokabiliwa na utapiamlo, na idadi hii imeongezeka kwa asilimia 50 kuliko mwaka jana.
 

Tuesday, December 13, 2016

Japan yatuma mtambo wa kufagia anga za juu

 

Japan imezindua chombo cha anga za juu ambacho kitabeba mtambo maalum wa kukusanya taka kutoka anga za juu.

Chombo hicho kitakuwa na nyaya ndefu za urefu wa mita 700 (nusu maili) ambazo zitatumiwa kuokota taka hizo. Nyaya hizo zitaundwa kwa madini ya aluminiamu na chuma cha pua.

Mtambo huo umeundwa kwa usaidizi kutoka kwa kampuni ya uvuvi.
Inakadiriwa kwamba kuna zaidi ya vipande 100 milioni vya taka kwenye mzingo wa dunia.
Mpango wa kupeleka watu wakaishi Mars
Kifaa kutoka angani chaanguka Myanmar

Vipande hivi ni pamoja na vipande vya setilaini zilizoacha kutumika, vifaa na vipande vya roketi.

Vipand vingi kati ya hivi vinasonga kwa kasi sana kuizunguka dunia kwenye mzingo wake, baadhi vikifikia kasi ya kilomita 28,000 kwa saa (maili 17,500 kwa saa) na kuna wasiwasi kwamba vinaweza kusababisha ajali mbaya au kuharibu mitambo inayosaidia mawasiliano duniani.
 
Taka hizo zimerundikana katika kipindi cha miaka 50 tangu binadamu aweze kuruka kwenya anga za juu, setilaiti ya Sputnik iliporushwa anga za juu na Muungano wa Usovieti mwaka 1957.

Mgongano kati ya setilaiti na kufanyiwa majaribio kwa mitambo ya kujikinga dhidi ya mshambulio ya setilaiti vimezidisha tatizo la taka anga za juu.


Chombo hicho cha Japani kimepewa jina Kounotori na kinaundiwa katika kituo cha anga za juu cha Tanegashima
 
Roketi ya H-IIB iliyobeba  chombo cha Kounotori ikipaa angani baada ya kurushwa kutoka kituo cha anga za juu cha Tanegashima tarehe 9 desemba



Chombo hicho kilichopewa jina Kounotori (Korongo kwa Kijapani) na ambacho kimebebea mtambo huo, kilipaa kutoka kituo cha safari za anga za juu cha Tanegashima, kaskazini mwa bahari ya Pasifiki Ijumaa kuelekea kituo cha kimataifa cha anga za juu.

Watafiti wanasema nyaya hizo zinazotumia nguvu za maalum za sumaku ambazo kwa Kiingereza huitwa electro-dynamic, kitazalisha nguzu za kutosha kubadili mwelekeo wa vipande hivyo na kuvielekeza kwenye anga ya dunia ambapo vitateketea.
Mataifa ya Ulaya kutuma chombo sayari ya Mars
Roketi kubwa ya Uchina yafanya safari ya kwanza

Kampuni ya wataalamu wa kuunda nyavu za kutumiwa na wavuvi Nitto Seimo Co, ambayo imekuwepo kwa miaka 106, imeshirikiana na shirika la anga za juu la Japan kuunda mtambo huo.

Majaribio ya kutumia mtambo huo ni moja ya juhudi za kuhakikisha anga za juu ni salama kwa wana anga kwa kupunguza taka.
Inatarajiwa kwamba itasaidia kulinga vituo vilivyo anga za juu pamoja na setilaiti za kutabiri hali ya hewa na zile zinazotumiwa kwa mawasiliano, vyote vya thamani ya mabilioni ya dola. Image copyright Getty Images

Waziri Nchemba: Maiti Saba wa Mto Ruvu ni wahamiaji haramu

 Mheshimiwa Mwigulu NCHEMBA (wewe ni waziri wa mambo ya ndani ya nchi)..,
.., leo asubuhi ulikuwa katika kipindi cha Tuongee Asubuhi kinachorushwa na kituo cha matangazo cha Star TV.., nimekusikia kauli zako, kuhusu 'issue' ya watu wale 7 waliokutwa mto Ruvu wakiwa wamekufa (vifo vya ajabu), umesema kwamba watu wale ni WAHAMIAJI HARAMU .., mimi nikuulize maswali yafuatayo;
(i) Je, wahamiaji haramu ndiyo wanapaswa kuuwawa na kutupwa mto Ruvu!?
(ii) wahamiaji haramu ndiyo wanapaswa kujeruhiwa kwa vitu vyenye ncha kali na kuuawa!?
(iii) wahamiaji haramu ndiyo wanatakiwa kuuwawa na kufungwa kwenye mifuko ya Sandarusi na kuwekwa mawe ndani!?
(iv) sheria za nchi, sheria za jeshi la polisi, sheria za idara ya uhamiaji zinasema nini kuhusu wahamiaji haramu.., kuuwawa!?
(v) kama kweli ni wahamiaji haramu.., nani ametoa idhini ya kuwaua, nani amewaua, na kwanini watupwe mto Ruvu wakiwa wamefungwa kwenye mifuko na mawe ndani yake!?
.., niendelee kukuliza mheshimiwa waziri.., hao wahamiaji haramu, wanatoka katika nchi gani.., Je, nchi zao zikigundua kwamba mliwaua watu wao na kuwazika huko Bagamoyo, hauoni mnaleta mgogoro mkubwa wa kidiplomasia!?
Mheshimiwa waziri, kazi ya jeshi la polisi ni kulinda watu na mali zao, kuhakikisha usalama wa raia ni kiwango cha juu, bila kuhatarisha usalama wao, maana wao ndiyo kipaumbele cha kwanza cha serikali (walipa kodi)..,
.., umetoa ufafanuzi hafifu sana kuhusu suala la kupotea kwa Ben Saanane na kutoonekana kwa kitambo kirefu.., kuna maswali ya kuoanisha hapa;
(i) kwanini ile miili 7 iliyokutwa kule Ruvu izikwe kwa haraka ile na halmashauri!?
(ii) kwanini jeshi la polisi, halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo hawakutaka kufanya uchunguzi kubaini nini chanzo!?
(iii) kwanini jeshi la polisi liko kimya hadi sasa, wiki nzima, hadi 'pressure' ya watanzania inakuibua wewe waziri, tena kwa kuulizwa!?
(iv) Je, wakati huu ndugu, jamaa, rafiki wa Ben Saanane wakiwa katika sintofahamu ya ndugu yao, kwanini Jeshi la polisi halikuona umuhimu wa kutokuzika maiti zile kwa haraka ile!?
(v) kuna kila sababu ya kumtaka OCD wa Bagamoyo na vyombo vya ulinzi na usalama katika halmashauri ya wilaya ya Bagamoyo, kutoa kauli yenye kueleweka.., (wako chini ya ofisi yako hawa watu)
NB; Pia.., kuna habari moja iliwahi kutangazwa na ITV mwezi wa August, mwaka 2016, naomba kunukuu sehemu ya habari ile..,
".., Zaidi ya watanzania 56 katika vijiji vya Chamchuzi na Buguluka vilivyoko katika kata ya Bwelanyange iliyoko wilayani Karagwe mkoani Kagera waliokuwa wakijihusisha na shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera na ziwa hiema wanadaiwa kutekwa na kuuawa kikatili na watu wanaodhaniwa kuwa ni askari wa nchi jirani Rwanda ambao mara kwa mara hufanya doria ndani ya mto huo na ziwa hilo. "
.., kitu cha kusikitisha sana.., serikali kupitia wizara ya mambo ya ndani ya nchi.., haikuwahi kutoa kauli, taarifa yoyote juu ya habari hiyo.., mbaya sana!
Mwisho ;
Jeshi la polisi kupitia intelejensia yake, wanapaswa kuwa 'proactive' kuliko kuwa 'reactive' kwenye masuala ya ulinzi wa mali za umma na usalama wa raia.., intelejensia ya jeshi la polisi inatakiwa kufanya kazi kubwa kabla umma kupiga kelele ndiyo wao wachukue hatua.., (kama jeshi la polisi linaweza kubaini kuhusu vurugu kutokea katika mkutano wa kisiasa ambao haujafanyika.., linashindwa nini kubaini usalama wa raia na mali zao!?)
matukio ya watanzania kuuwawa yamekuwa yakiongezeka kila kunapokucha, watanzania 9 katika wilaya ya Kyelwa waliokuwa wakifanya shughuli za uvuvi ndani ya mto Kagera waliuwawa na watu wanaodhaniwa askari wa nchi jirani ya Rwanda hali ambayo ilikusikitisha wewe (waziriwa mambo ya ndani) wakati huo ukiwa katika ziara ya kikazi katika mkoa wa Kagera.., (lakini wizara yako haikutaka kutoka mbele ya watanzania na kusema kitu, kuhusu matukio hayo)
Jeshi la polisi linapawa kuwa jeshi la kulinda raia na mali zao.., siyo jeshi la kulinda maslahi ya watu wachache sana katika Jamhuri ya muungano wa Tanzania.., tazama, raia wanakufa vifo vya ajabu katika nchi yao, zinatoka kauli rahisi, kwamba ni wahamiaji haramu.., siyo sahihi.., tunapaswa kupata ukweli dhidi ya maiti zile zilzokutwa katika mto Ruvu.., pia tuelezwe;
(i) kwanini zitupwe mto Ruvu.
(ii) kwanini zifungwe na mawe ndani.
(iii) kwanini zifungwe katika mifuko ya Sandarusi.
(iv) kwanini zionekane kujeruhiwa na vitu vyenye ncha kali.
(v) kwanini mamlaka za usalama ziko kimya..,
Ahsante,
Mwananchi wa kawaida,
Martin Maranja Masese (MMM)
Source JF
waziri wa mabo ya ndani Ndg Mwigulu Nchemba

Monday, December 12, 2016

CHAMBUA MATAMKO YAFUATAYO...

#PART ONE:
1. WAZIRI WA VIWANDA, MWIJAGE "...tulikuwa tunaficha tu, ukweli ni kuwa DANGOTE anataka apewe GESI bure, nchi hii siyo shamba la Bibi"
2. WAZIRI WA NISHATI, MUHONGO "...DANGOTE hawasemi ukweli, gharama na Makaa ya Mawe ya Tanzania ni nafuu kuliko ya Afrika Kusini, hebu naomba wawaeleze ukweli"

3. TPDC: "...Shirika la Maendeleo la Petroli Tanzania (TPDC) linapenda kukanusha taarifa zinazoenezwa na Kampuni ya Dangote pamoja na washirika wake kupitia mitandao ya kijamii.....Kiwanda cha Dangote kimeomba kupewa gesi asilia kwa bei ambayo hapa kwetu Tanzania ni kidogo kwani kiasi hicho cha bei ndicho kinacholipwa kununulia gesi ghafi kutoka kisimani.... Taarifa hizo (Za Dangote) hazina mantiki yoyote na zinapaswa kupuuzwa...."

4. RAIS JPM: "...Kuna ujanja ujanja unatumika kumuuzia GESI Dangote kwa faida ya wachache, kuanzia sasa wasiliana na serikali moja kwa moja...."

5. DANGOTE: "...Hapakuwa na tatizo lolote, kila kitu kinakwenda sawasawa...".
#PART TWO:
1. WAZIRI MWIGULU NCHEMBA: "...miili iliyookotwa ni ya wahamiaji haramu..."

2. WAZIRI MKUU, KASIMU MAJALIWA: "Miili iliyookotwa inahusishwa na masuala ya Ugaidi..."
3. WAZIRI MKUU, KASIMU MAJALIWA: "Naagiza Uchunguzi mara moja (akiielekeza Wizara ya Mwigulu".

SOMO LA MAISHA KUTOKA KWENYE WARAKA WA SERENA

VITA ya ubaguzi wa kijinsia kwenye malipo ya wacheza tenisi imepamba vyombo vingi vya habari mwanzoni mwa mwaka huu, huku mmoja wa nyota wa kike wa mchezo huo waliopigia kelele sana suala hilo, Serena Williams, akizidi kulivalia njuga.

Moja ya mfano aliotoa Serena kuonyesha kuna ubaguzi wa kijinsia kwenye mchezo huo ni pale wanapomtaja kama mwanamichezo bora wa kike, badala ya kusema mmoja wa wanamichezo bora.

Mshindi huyo wa mataji makubwa 22, ameweka wazi kuhusiana na hilo kwenye barua yake ya wazi iliyochapishwa na jarida la Porter.

Mwanzoni mwa mwaka huu, mchezaji wa zamani wa tenisi, Ray Moore, ambaye pia ni mwandaaji wa michuano mbalimbali ya mchezo huo kama Paribas Open, California, alisema kwamba wachezaji wa kike wa mchezo huo wanapaswa kuwashukuru Roger Federer na Rafael Nadal kuubeba mchezo huo.

Lakini Serena alimpinga wazi mkongwe huyo mwenye umri wa miaka 70, kabla ya baadaye kuandika waraka mkubwa.

Serena aliandika katika waraka wake: “Nimekuwa na bahati kuwa kwenye familia ambayo inaunga mkono ndoto zangu na kunitia moyo.”

“Nimejifunza kutokuogopa. Nimejifunza umuhimu wa kupigania ndoto zangu, jambo la msingi likiwa ni kufikiria makubwa zaidi. Vita yangu ilianza nikiwa na umri wa miaka mitatu na tangu hapo sijakata tamaa.

“Lakini kama tunavyojua, mara nyingi wanawake hawapewi kipaumbele cha kutosha au kukatishwa tamaa kwa kile wanachokichagua. Naamini pamoja tunaweza kubadilisha hilo. Kwangu mimi ilikuwa ni suala la ujasiri.

“Kile wengine walichoona kama ni kosa au kutokuwa na faida, lakini kwa upande wangu, vita yangu, jinsi yangu vilichochewa na mafanikio yangu. Kamwe sikuruhusu kitu chochote au mtu kunifanya nishindwe.

“Wakati suala la kulipwa sawa na wanaume linapokuja, linanikera sana kwa kuwa najua kila kitu kama mtu mwingine, tumefanya kazi moja na kujitoa sawasawa kama wanavyofanya wanaume. Sitapenda binti yangu alipwe kidogo kuliko mtoto wangu wa kiume kwa kazi moja wanayoifanya. Au wewe utapenda. Siwezi kunyamaza.”

Pia Serena alishangaa suala la kuingiza jinsi yake kwenye kutaja mchezo wake kati ya wachezaji wengine, huku Federer akiwekwa pamoja na mchezaji wa gofu Tiger Woods na nyota wa mpira wa kikapu, LeBron James.

“Kama mnavyojua wanawake wanapitia vikwazo vingi mpaka kuweza kufikia mafanikio,” aliandika Serena.

“Vikwazo vinaendelea kuwapo siku zote kwa wanawake. Watu huniita wa wanamichezo wakubwa wa ‘kike’ duniani.’ Je, wanasema LeBron ni mmoja wa wanamichezo bora wa kiume? Vipi kwaTiger? Federer? Kwanini wao wasiitwe hivyo? Kwa kuwa wao si wa kike. Tuhukumiwe na mafanikio yetu sio na jinsi zetu.

“Katika kila kitu nilichofanikiwa kwenye maisha yangu, nashukuru nimepitia milima na mabonde ambayo inakuja na mafanikio. Ni matumaini kwamba historia yangu na ya kwako itawatia moyo wanawake wengi kupambana kwa ajili ya mafanikio na kutimiza ndoto zao. Lazima tuwe na maono makubwa ili kukitia moyo kizazi kijacho cha wanawake ili kuweza kupambana.”
 

Wednesday, December 7, 2016

Waziri wa afya wa Tanzania atahadharisha juu ya mlipuko mpya wa kipindupindu

Waziri wa afya wa Tanzania Bw Ummy Mwalimu ametahadharisha kuhusu mlipuko mpya wa ugonjwa wa kipindupindu nchini humo.

Bibi Mwalimu amewataka maofisa wa afya kutekeleza taratibu zinazolenga kusimamia maambukizi ya ugonjwa huo na kuanzisha kampeni ya kuelimisha umma kuhusu ugonjwa huo.

Ripoti mpya iliyotolewa na wizara hiyo inaonesha kuwa watu 6 wamefariki dunia na wengine 458 wameripotiwa kuambukizwa ugonjwa huo mwezi Novemba, na maeneo yaliyoathiriwa zaidi na Morogoro, Dodoma, Mara, Kigoma, Arusha na Dar es Salaam.
Bibi Mwalimu amesema ugonjwa huo hutokana na uchafu, na baadhi ya watu wana desturi ya kuchafua vyanzo vya maji.

waziri ummi akizungumza na waandishi wa habari

MATAPELI WAKUBWA WANNE (4)KUWAHI KUTOKEA TANZANIA : 

 
1..DAUDI BALALI... Nahisi huyu ni mmoja kati ya watanzania magenious zaidi kuwahi kutokea. Huyu kipindi anasoma alirushwa sana madarasa kutokana n kiwango kikubwa cha akili. Hii ilipelekea yeye kusoma elimu ya msingi na secondary kwa miaka 10 tu. Akiwa na miaka 18 alijiunga na chuo kikuu cha Howard marekani ambapo alitunukiwa shahada yake ya kwanza. Akiwa na miaka 25 alitunukiwa PHD.. Kisha akarudi nchini kuwa mchumi wa bank kuu mwaka 1967.. Baadae kidogo akaajiliwa IMF ambako alifanya kazi kwa miaka 23 kabla ya mkapa kumrudisha nchini kama mshauri wake wa masuala ya uchumi na baadae kumfanya gavana wa bank kuu.
Kilichofanya kuwepo kwenye list hii ni tukio alilofanya la ukwapuaji wa BILLION 164 za kitanzania pale bank kuu..
Nafahamu kuna theories nyingi sana kuhusu ufisadi wa EPA lakini kwa mujibu wa serikali ni kuwa BALALI alikula njama yeye na wale wafanyabiashara wakakwapua fedha pasipo serikali kujua, kwa maana hiyo BALALI alimpiga changa la macho Waziri mighiro, Rais, na hata usalama wa taifa..... ALIWEZA
2..MANYAUNYAU
Huyu jamaa tunafahamu alitikisa sana miaka ya 2006 hadi 2008 alijigamba kuwa akinywa damu ya Paka anapta uwezo wa kimiujiza kufichua wachawi. Alizunguka mitaa karibia yote ya uswahilini dar (uzunguni alipatenga) baada ya kuteka Hisia za watu vya kutosha akaanza na ziara za mikoani.
Jamaa akaingiza mkwanja mrefu sana kwa kazi yake hii nakumbuka miaka ile ya 2008 alishanunua RAV4 Kali na mjengo wa maana.... Sijui kwa sasa amepotelea wapi!
3..ALEX MASSAWE
Huyu jamaa ni tapeli(first class) alikuwa anatapeli kuanzia raia wenzake, serikali, mashirika mpaka matajiri wakubwa. Alitapeli sana watu nyumba, magari, mashamba na hata fedha, serikali iliangaika sana na huyu jamaa kwa miaka kadhaa lakini hawakufua dafu, mpaka interpol walipomkamata huko dubai.
Inasemekana jamaa alikuwa a napiga dili zake na watu wazito serikaln na bungeni. Inasemekana kuna wabunge watatu kutoka mkoa mmoja wa kaskazini ndio alikuwa anapiga nao sana ishu za madili ya gari za wizi na kusafisha fedha haramu..
4..BABU WA LOLIONDO
Mpaka Leo hii bado sijaelewa babu aliwezaje kuwapiga changa kiasi Kile, hivi ni kwamba babu alikuwa kichwa sana au media ilisaidia. Kipindi kile kuna watu walitamani BABU atangazwe kama nabii au shujaa wa taifa, mpaka wa kuu wa nchi walitengeneza hadi kiwanja kidogo cha ndege wakawa wanatua, wanapanga foleni, wanapiga magoti kwa unyenyekevu na kuachama midomo kama wanakula sakramenti takatifu.. Kila Kona ilikuwa BABU, BABU, BABUUUUU...
kila mtu kuanzia raia hadi viongozi wakubwa walikuwa wanapigania KIKOMBE kwa mchango (sadaka) ya mia tano tano (500)na ghafla ikawa ziiiiii Babu kimyaaaa




matukio ktk picha
 
GODBLESS LEMA......
https://www.facebook.com/100008744220984/videos/1628725077428951/

Thursday, December 1, 2016


UFAFANUZI WA KAULI YA PAUL MAKONDA.

Na:Goodluck Abel 
"Msinijaribu, ardhi kinondoni nitawashughulikia, hadi mtajuta kuzaliwa. 'Mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu', sikuletwa hapa kwa bahati mbaya, nitawatia ndani wote, na hakuna mtetezi wenu, wewe mama unanisikia? hauna wa kukutetea.."

Kauli hiyo imetolewa na kijana wa UVCCM aliyeteuliwa na Rais Magufuli kuwa mkuu wa mkoa wa Dar es Salaam ili kuwakomesha wapinzani, Ndg. Paul Makonda.

Ili kuelewa, ni vema kutafakari neno kwa neno, kama ifuatavyo;

1. "Mtajuta kuzaliwa", kujuta kuzaliwa ni hatua ya mwisho ambayo binadamu huifikia hata akamuuliza muumba wake ni kwanini alimuumba, hivyo Makonda anajivika cheo cha muumbaji.

2. " Hakuna wa kuwatetea", kwamba akiamuru yeye, maamuzi yake ni ya mwisho. Lakini katiba na sheria za nchi zinamruhusu mtu kujieleza (natural Justice), na kuwa na utetezi dhidi ya mashitaka yake mahakamani, hivyo: kwa amri ya Makonda, akikuweka ndani unaweza kuozea huko na hakuna wa kukutetea.

3. "Nitawashughulikia", maana yake atatoa adhabu, ambapo katiba ya nchi inasema kuwa mtu hatoadhibiwa kwa kosa lolote, hata la jinai, mpaka itakapothibitika mahakamani kuwa ana kosa, hivyo: Makonda ndiyo mwenye mamlaka na maamuzi ya mwisho juu ya hukumu ya mtu na sio mahakama tena.

4. " Mimi nikisimama hapa, amesimama Mungu", #Astaghfirullah... Yaani Makonda sasa anachukua nafasi ya Mungu, kwa hili nashindwa kufafanua zaidi, naishia kutamka tena 'Astaghfirullah' yaani 'Mungu asamehe'.

5. "Sikuletwa hapa kwa bahati mbaya", hili: kwa bahati mbaya hatufahmu kuna nini nyuma ya pazia hata yeye mwenyewe kukiri kuwa hakuletwa kwa bahati mbaya, maana yake lipo kusudi, na matokeo ya kusudi hilo ni hayo yaonekanayo, mbali na aliyemteua kusema kuwa "nimekuongeza cheo ili kuwakomesha wapinzani wako"

Hapa ndipo tulipofikia mtanzania mwenzangu, tufahamu kuwa nchi yetu ikiupoteza utawala bora unaozingatia sheria za nchi na katiba yetu wenyewe, nchi itatumbukia pabaya siku za usoni.


TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI;

Imetolewa na Afisa mawasiliano na Uchaguzi –CUF TAIFA, 29 Novemba 2016.

"DHAMBI YA USALITI INAMTESA LIPUMBA".

Jana tarehe 28/11/2016 Lipumba alizungumza na waandishi wa habari kwa kile alichokiita kujibu hoja za Katibu Mkuu wa Chama Maalim Seif Sharif Hamad alizotoa katika mkutano na wahariri na waandishi wa vyombo mbalimbali vya habari vya ndani na nje ya nchi.
Tunasikitika kusema kuwa Lipumba ameshindwa kujibu hoja na badala yake amejikita kwenye majigambo na kujifaharisha na waganga wa kienyeji na vyombo vya dola kuwa wamemuhakikishia ataendelea kuwa Mwenyekiti wa CUF mpaka mwaka 2019.

Kwanza tunawashukuru watanzania kwa kuendelea kumpuuza kwani yapo masuala mengi yanayowasumbua watanzania kama kuyumba kwa uchumi na serikali ya awamu ya tano ambayo Lipumba alijenga ubia nayo tangu kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka jana ikiwa ni pamoja na mwendelezo wa urafiki wa kuihujumu CUF.

Ndiyo maana hivi sasa anashindwa kufungua mdomo wake kukosoa na kushauri hadhara njia mbadala za kuondokana na hali hii badala yake anampongeza Mheshimiwa Rais Magufuli na serikali yake kwa kuharibu uchumi wa nchi. Lipumba huyu siyo yule tuliyekuwa tunamfahamu. Na haya ndiyo madhara na gharama ya kuwa kibaraka wa mfumo kandamizi wa demokrasia.

Ameshindwa kujibu hoja na ameshindwa kukanusha juu ya uhusiano wake na Jeshi la polisi nchini ambao umekuwa ngazi ya kuhujumu Chama huku vitendo vya kihalifu vya Lipumba na wapambe ake vikikingiwa kifua. Amejitwika jukumu la kuwa msemaji wa Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa nchini na kushindwa kupinga hoja ya jaribio la kutaka kuiba fedha za ruzuku za Chama kwa kutaka kufungua akaunti binafsi akishirikiana na Jaji Francis Mutungi. Ameshindwa kujibu hoja kuwa wapambe na wahuni wake wanafanya uhalifu na kulindwa na Polisi na bila kuchukuliwa hatua zozote. Lakini pia hajawaambia Watanzania sababu za kujiuzulu kwake na sababu za kutaka kulazimisha tena kuendelea kuwa Mwenyekiti wa The Civic United Front (CUF-Chama Cha Wananchi).

Lipumba anajidhalilisha na kujivunjia heshima na mwenye njaa ya ruzuku ni yeye aliyetaka kufungua akaunti yenye jina la chama ili ajichukulie fedha za chama kinyume na taratibu na hali akijua hana mamlaka ya kufanya hivyo.

Hata kama angekuwa ni ‘Mwenyekiti Halali wa Chama’ kwa mujibu wa Katiba ya CUF; Majukumu ya Mwenyekiti wa Chama Taifa yamebainishwa katika ukurasa wa 82 Ibara ya 91(1)(a-m) ambayo hayampi mamlaka ya kufanya haya anayoyafanya Lipumba ikiwemo kutaka kudhibiti fedha na mali za Chama.

Katiba ya CUF ambayo yeye anadai na kusisitiza kutaka ifuatwe kwa kuiangalia zaidi Ibara ya 117(2) pekee, imempa Majukumu muhimu Katibu Mkuu wa Chama katika ukurasa wa 85 Ibara ya 93(1)(a-k)(2) kuwa;
a) “Atakuwa Mtendaji Mkuu wa Chama na pia mwajibikaji mkuu wa shughuli zote za utendaji za Chama kitaifa” Ibara ya 93(1)(a).

b) "Atakuwa na dhamana ya ofisi za Makao Makuu na Ofisi Kuu ya Chama” Ibara ya 93(1),(f)

c) "Atakuwa mwajibikaji mkuu wa mambo yote ya fedha na mali za Chama katika ngazi ya Taifa (Chief Accounting Officer)” Ibara ya 93(1),(i).

Kwa hiyo, kitendo cha Katibu Maalim Seif, kuhoji juu ya UHUNI wa Jaji Mutungi wa kuzuia RUZUKU ya CUF kwa sababu Mutungi aliona haitamfikia Lipumba ili kutumika kwa malengo ya dola kuisambaratisha CUF, ni kitendo muhimu sana kikatiba, ni kitendo kinachodhihirisha kuwa Katibu Mkuu anatimiza wajibu wake kama Msimamizi Mkuu wa masuala ya fedha za chama. Kama ni njaa anayo BWANA YULE, ambaye alipokwenda Lindi na Mtwara alibeba vimemo na kuingia benki ya NMB tawi hatulitaji na kupewa Tzs 20,000,000 kwa maelekezo ya kada na kiongozi maarufu wa CCM. Wafanyakazi wa Tawi hilo la NMB hadi leo hawaamini inakuwaje kiongozi wa Upinzani aliyejitambulisha kama anayepambana na CCM, kupewa mamilioni ya pesa na viongozi wa CCM.

Njaa! Kama kuna mwanasiasa ana njaa na ametumia maisha yake kutumika ni Lipumba. Lipumba na wahuni wake wakumbushwe juu ya hotuba zake mwaka 2011 baada ya Kikwete kushinda ushindi mwembamba. Lipumba hajawajibu watanzania alikuwa na maana gani kusema "aliokoa jahazi ili Kikwete ashinde uchaguzi" ilihali Lipumba alikuwa mgombea wa CUF. Je,ni kikao gani cha CUF kilimtuma Lipumba akaokoe jahazi na kumpa ushindi Kikwete mwaka 2010?

Lipumba amepoteza weledi wake wa mambo tuliokuwa tunaujua hapo kabla, anazungumza mambo bila Takwimu, bila ushahidi. CUF kama taasisi makini, taasisi Imara imeshafanya maamuzi kupitia vikao halali vya Chama Mkutano Mkuu Taifa na Baraza Kuu la Uongozi Taifa, Katibu Mkuu Maalim Seif Sharif Hamad hana mamlaka ya kuzungumza na Lipumba na kulipatia ufumbuzi suala hili kwa kuwa si lake ni la Chama na Chama kilishafanya maamuzi ya kumvua uanachama. Kazi aliyojipa kwa kupewa bahshishi na washirika wake ya kuvuruga upinzani haitafanikiwa kwa sababu CUF na vyama washirika itaendeleza ushirikiano na kuondoa mapungufu yote yaliyojitokeza katika uchaguzi uliopita ili tuwe na nguvu madhubuti ya pamoja kukabiliana na CCM katika chaguzi zijazo. Kamwe hataweza kuturudisha nyuma na kutuyumbisha.

Lipumba anazungumzia ujumbe wa Maalimu Seif kupitia barua pepe yake ya Disemba 30, 2015 eti kuwa anamtambua! Hii inatia shida kidogo kumuelewa Lipumba, alisema ataendelea kuwa mwanachama wa kawaida na kadi yake amelipia mpaka mwa 2020, sasa kutumiwa ujumbe ndio imemaanisha kuwa yeye ni ‘Mwenyekiti Halali’ na inadhihirisha kuwa Maalim Seif hana ugomvi binafsi yeye. Inastaajabisha sana kuona kuwa aliyekuwa kiongozi wa kupinga propaganda za CCM leo anatumia propaganda hizohizo dhidi ya Chama cha CUF kutaka kuwabagua watanzania kwa misingi ya udini, ukanda, utanganyika na uzanzibari.

Wakati Maalim Seif anajenga hoja za matukio takribani tisa yaliyotokea katika kipindi cha baina ya Mwezi Agosti-Novemba, 2016 ikiwemo jaribio la utekaji na Jeshi la Polisi kushindwa kutekeleza wajibu wake, yeye amejitokeza kuwa msemaji pia wa jeshi la Polisi, kwa kweli inasikitisha sana. Lipumba aache kuwa na uchu wa madaraka zama zake zimekwisha ndani ya CUF, kutamani kwake kugombea nafasi ya Urais mwaka jana kuliathiriwa na hali halisi ya mazingira na haja ya wakati ule na hayakuruhusu kabisa kwake kuwa mgombea na kufanya vizuri. Eti Lipumba haoni mchango wa Mhe. Edward Lowassa katika UKAWA! Je? Dhamira na nafsi yake zimeacha kumsuta? Mhe. Edward Lowassa amepata asilimia 39 ya kura, Lipumba anakataa kuwa Lowassa hana mchango kwenye mabadiliko ya demokrasia nchini? Lipumba alizoea kupata asilimia 7 ya kura na alijenga ufalme akidhani kuwa ataendelea kuwapiga mnada watanzania na kuchukua hela ili "kuokoa ahazi" kila chaguzi utakapofika?

Kwa upande wa Zanzibar CUF tumeshinda nafasi ya Urais na kushuhudia CCM na Dola wakipora ushindi huo kwa kumtumia Mwenyekiti wa Tume ya Uchaguzi Zanzibar –ZEC. Lipumba anakataa? Anaunga mkono maamuzi ya mwenyekiti wa Tume ya uchaguzi Zanzibar ZEC? Lipumba anachukia ikielezwa kuwa Mhe. Edward Lowassa amemshinda Magufuli katika matokeo ya kura za Urais Zanzibar!

Kushirikiana na vyama vingine vya siasa ni maamuzi yanayotokana na kikao cha Baraza Kuu la Uongozi la Taifa ambalo bado linatambua uwepo wa ushirikiano wa vyama–UKAWA. Je yeye binafsi kama angekuwa Mwenyekiti wa CUF Taifa anao uwezo wa kuiondoa CUF katika UKAWA bila kutumia njia za vikao? Mashirikiano haya yanaendelea katika uundaji wa Halmashauri na CUF kuwa na Mameya na Manaibu Meya Je kwa akili ya Lipumba Mameya na Manaibu Meya hawa wajiuzuru ili wasishirikiane na CHADEMA? Aleze sababu za kulazimisha kutaka kuwa mwenyekiti ni zipi wakati alijiuzuru kwa matashi yake binafsi mbali na kuombwa asifanye hivyo? Iweje viongozi wa Dini na wa Chama waliomuomba sana wakati ule asijiuzulu akawakatalia katakata na kuendelea na dhamira yake na hatimaye akakimbia vita na kukiacha chama katika kipindi kigumu cha maandalizi ya uchaguzi mkuu, ilhali leo anadai amezingatia maombi ya viongozi wa dini wale aliowakatalia mwanzo? anadai kuwa alimuandikia barua Katibu Mkuu akajibiwa kuwa asubiri, kwani kwa akili ya Lipumba, kurudi kwake kwenye nafasi ya Uenyekiti wa Chama kwa mujibu wa katiba ya CUF yanafanywa na Katibu Mkuu wa Chama? Huu ni umbumbumbu wa sheria na Katiba ya CUF wa hali ya juu.

Kwa mashirikiano ya CUF na vyama vingine tumeweza kufanya kampeni za uhakika na za kisasa zilizoleta ushindani mkubwa na kuifanya CUF ipate wabunge katika majimbo kumi (10) ya Tanzania Bara na kuongoza Halmashauri nne (4) nchini. Lipumba anakataa na kupinga kuwa hatukupata wabunge 10? Je, anakumbuka kuwa miaka yake 19 ya Uenyekiti wa CUF chama hakikuwahi kuwa na wabunge hata watatu? Leo CUF ina halmashari 4 na madiwani zaidi ya 300, miaka 19 ya Uenyekiti wa Lipumba ndani ya CUF iliwahi kuleta hata halmashauri moja?

Lipumba ametakiwa aeleze sababu za kujiuzuru kwake ni zipi? lakini ameshindwa kufanya hivyo. Lipumba anazeeka vibaya na amekuwa msahaulifu, anapozungumza katika vikao vyake vya ndani maeneo mbalimbali anasema Wazanzibar hawamtaki na kwamba wanataka kujitoa katika makucha ya Wazanzibari, anazungumzia Utanganyika na Uzanzibari, na wapambe wake wanalishikilia bango suala hili. Aache kueneza na kupandikiza chuki kwani ajenda hizo ndizo zimefanya miaka yake 19 ya uongozi ndani ya CUF kukosa lolote la kujivunia.

KUHUSU SUALA LA UMOJA WA KATIBA YA WANANCHI-(UKAWA):

Lipumba ameulizwa na kushindwa kujibu, nani aliyeleta UKAWA ndani ya CUF? Nani aliyeweka saini za makubaliano ya UKAWA pale Jangwani? UKAWA umeanzia Bunge la Katiba. Katibu Mkuu Maalim Seif hakuwa mjumbe wa Bunge la Katiba. Yeye Lipumba ndiye aliyekwenda kumuona Mheshimiwa Lowassa na kumtaka ikiwa CCM itamuengua ajiunge na UKAWA. Akashauri ajiunge na NCCR–Mageuzi na CHADEMA na CUF tumuunge mkono. Ni yeye aliyemtambulisha Lowassa kwa waandishi wa Habari. Lipumba anajaribu kuiweka CUF sokoni, ili iinunue na itumiwe kuudhoofisha upinzani.

Lipumba amezoea na ameshaonja radha ya kutumika, alitumika mwaka 2010 akamsaidia Kikwete kushinda urais, mwaka 2015 alipoona hawezi kugombea urais akajua wanunuzi wataona hana thamani, akaona njia ni kujitoa kwenye chama ili wanachama wavurugike, mpango wake ukafeli vibaya kwani CUF ni taasisi. Wanunuzi wake, CCM, waanze kutafuta bidhaa nyingine kwa sababu CUF ilishamalizana naye. Waendelee kumpa ulinzi wa defender’ za Polisi, wampigie Saluti, wampe uenyekiti wa chama kwa nguvu ya dola n.k. Yote hayo hayataihamisha CUF kwenye ajenda zake katika kuwapigania Watanzania na Wazanzibari kwa ujumla.
Na mwisho sote tunaweza kuendelea kujiuliza swali la msingi, ni mahali gani Duniani kiongozi wa juu wa taasisi kubwa kama CUF ambaye aliwahi kuandika barua ya kujiuzulu na kuiacha ofisi yake kwa muda wa miezi kumi, taasisi ikachagua au kuteua kiongozi mbadala wa nafasi hiyo kisha baadae mtu huyo akalazimisha kurejea katika nafasi yake?

Mwisho:

Tunamtaka Lipumba ajiheshimu na kuacha kujidhalilisha kwa kulazimisha mambo ambayo hayawezekani na yaliyo kinyume na matakwa ya Katiba ya CUF. Chama chako kikishakukataa ndani ya chama, hata kama ungekuwa,na majeshi kutoka mwezini, huwezi kuwa kiongozi wa chama hicho. Tunamtahadhalisha Lipumba na wahuni wake kuwa watabeba Msalaba wa gharama zote zitakazotokana na uharibifu wowote wa mali za Chama utakaojitokeza. Yeye si wa kwanza kujaribu kutumika kutaka kuvuruga CUF na au vyama vya upinzani nchini lakini wote waliotumika muda wa kutumika ulipokwisha walitelekezwa na kufedheheka. Lipumba ashughulikie masuala yanayohusiana na fani yake ya uchumi kama alivyoaihidi wakati anajiuzuru, siasa imemshinda.

CUF imevuka vigingi vingi vizito katika nyakati tofauti kila ilipojaribiwa ikiwa kwa uadui wa ndani au wa nje, mwisho wa vitimbi vyote hivyo, CUF iliibuka mshindi. Tunatoa wito kwa wanachama, wapenzi wa CUF, na watanzania wote kwa ujumla waendelee kuwa na Subira. Hakika CUF ni taasisi makini na imara ya kisiasa nchini, na mwisho wa hili CUF ndiyo itakayoshinda.

"HAKI SAWA KWA WOTE"

YOWERI K. MUSEVEN HAS MOCKED HUMANITY

Yoweri Museveni has mocked humanity the manner in which history has never written before. We beseech the rest of the world to beware of nations run from the bedroom of a dictator.
 

Mwishoni mwa wiki iliyopita, watu zaidi ya 80 walipoteza maisha baada ya makabiliano kati ya walinzi wa Mfalme wa eneo la Rwenzururu Charles Mumbere na maafisa wa usalama.Je, hili ni tatizo la kisiasa ua kiusalama ? Victor Abuso anachambua suala hili kwa kina na Kenneth Lukwago akiwa jijini Uingereza na Brian Wanyama Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Kibabii mjini Bungoma nchini Kenya.

 




picha za tukio la mauaji nchini Uganda
 

Wednesday, November 30, 2016

MSIBA MZITO KATIKA MPIRA WA MIGUU DUNIANI

ForçaChapecoense

Uongozi wa Naipenda YANGA unajumuika na wapenda mpira wa miguu duniani kote kutoa simanzi zetu pamoja na mkono wa pole kwa klabu ya Associação Chapecoense de Futebol ya nchini Brazil ambayo imepoteza viongozi wa klabu, benchi zima la ufundi na wachezaji wote 22 (wamepona wawili tu, ambao wako Hospital) waliopata ajali ya ndege nchini Colombia.


*** HISTORIA FUPI YA CHAPECOENSE ***

Ikiwa imeanzishwa mwaka 1973, ilishiriki mara ya kwanza Ligi Kuu ya Brazil, maarufu kama Serie A mwaka 2014, ikiwa imepanda daraja mfululizo kuanzia Serie D mwaka 2009.

Mwaka huu ilifanikiwa kupata uwakilishi kucheza michuano ya Copa Sudamericana (sawa na CAF Confederation Cup ya Afrika au UEFA Europa League ya Ulaya) na ikafanikiwa kutinga fainali kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Ikiwa njiani kuelekea nchini Colombia kucheza mechi ya kwanza ya fainali dhidi ya Atletico Nacional ya huko , ndege iliyowabeba yao ilipata ajali kutokana na hitilafu ya umeme na kuanguka karibu na mji wa Medellin, Colombia.

*** MSAADA KWA CHAPECOENSE ***

Klabu zote kubwa nchini Brazil, zimetoa mapendekezo yao kwa Shilikisho la Soka nchini Brazil ikiwa ni jitihada zao kuisaidia timu ya Chapecoense kujijenga upya wakati huu ambapo hawana wachezaji karibu wote, pamoja na benchi zima la ufundi.
Klabu hizo ambazo ni Corinthians, Santos, Sao Paulo na mabingwa wapya Palmeiras, wamewasilisha mapendekezo yafuatayo . . . .
1. Kuipa kinga maalum timu hiyo isishuke daraja kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia sasa mpaka itakapojijenga tena upya

2. Kuruhusu klabu yoyote kutoa wachezaji BURE kabisa kwa msimu ujao wa 2017 ili waweze kucheza mechi zao kwa ushindani
- Klabu hizo zimesema zipo tayari kutoa wachezaji wake muhimu wakachezee Chape.

Klabu ya Atletico Nacional ambayo ilikuwa icheze nayo fainali, imeiomba shirikisho la soka la Amerika ya Kusini kuitangaza Chapecoense kama Mabingwa wapya wa Copa Sudamericana 2016, kwa heshima yao kipindi hiki kigumu kwao.

Klabu ya PSG ya Ufaransa tayari imetangaza kutoa Pauni Milioni 40 kusaidia kuijenga upya kikosi cha Chapecoense.


picha zote tatu ni mabaki ya ndege iliyopataajali na kuuwa zaidi ya watu 72
 

Tuesday, November 29, 2016

'Tafuna pesa zao Bastian'

Bastian Schweinsteiger ameambiwa kwamba awaadhibu Manchester United kwa kuutumikia mkataba wake mpaka mwisho wa siku yake.

Kiungo huyo mshindi wa kombe la Dunia amekuwa kwenye wakati mgumu kwenye kikosi cha Jose Mourinho mpaka kushindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha ligi ya Europa.

Hivi karibu Mourinho alimjumuisha Bastian kwenye kikosi cha kwanza Man United lakini bado hajacheza hata mechi moja kuelekea miezi yake 18 ya mwisho wa mkataba wake.

Sasa, Rais wake wa zamani katika klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness amemshauri kwamba achukue kila salio la pesa kutoka Man United kabla ya kuachana na soka .

"kama ningekuwa mimi,ningewakomesha watu wa Manchester wanilipe mpaka mwisho wa mkataba wangu"

"Hicho ndio klabu kama hii inastahili kufanyiwa kwa kile wanachomfanyia. Lazima waadhibiwe."

Mapema mwaka huu Schweinsteiger alisema kwamba Manchester United itakuwa klabu yake ya mwisho barani Ulaya na kuibua tetesi kwamba huenda akahamia Major League Soccer. Lakini Hoeness alisema," kwa nilichokisikia, Basti anaelekea kuachana na soka, namjua vizuri sana nina mashaka sana kama bado ana moto wa kukabiliana na changamoto nyingine tena 
 
 

WIZARA YA ELIMU YAKANUSHA MATAMKO YA WAZIRI NDALICHAKO.


Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia imekanusha taarifa zilizoenea ya kuwa, Waziri wa Elimu Prof. Ndalichako amezuia wanafunzi wenye Stashahada (Diploma) kujiunga na masomo ya Shahada (Degree) katika vyuo vikuu.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Naibu Waziri wa Elimu, Mhandisi Stella Manyanya amesema kuwa, katazo lililotolewa na Waziri Prof. Ndalichako siku ya mahafali ya Chuo Kikuu Huria cha Tanzania linawahusi wale tu wanaosoma Foundation Courses ili kuweza kujipatia sifa za kujiunga na chuo kikuu.
Taarifa imeeleza kuwa awali wanafunzi ambao walifeli kidato cha nne walikuwa wakisoma Foundation Courses katika vyuo mbalimbali na kisha kujipatia sifa za kujiunga na chuo kikuu kitu ambacho waziri alisema sasa hakitakuwepo tena.

Utaratibu huu ulikuwa ukitumika zaidi katika Chuo Kikuu Huria ambapo wanafunzi walikuwa wakisoma programu maalum zilizokuwa zikiwapa sifa ya kusoma Shahada.

“Kilichojitokeza ni kuna taarifa zinasambaa kwamba kuanzia sasa wanafunzi watakaoenda chuo kikuu ni wale ambao tu wamepitia form six sasa hiyo taarifa imeleta presha kubwa, nimekuja hapa sio kukataa tamko hilo hapana nimekuja kulitolea ufafanuzi.”

– Naibu Waziri Eng. Stella Manyanya
 
Huu mwenendo wa kulopoka na bila kua na mpangilio wa kina wa agenda husika, unaigharimu wizara hii na zingine, kila wakati kujitokeza kufafanua anachoongea boss wao. Kwani wanapokua wanatoa matamko mnakua hamjaongea kwa makubaliano kama wizara au kuna nini? Mjipange aisee msituone kama vile hatujui kiswahili ndio maana mnasubiria aongee alafu mje muwe wakalimani.
 
 

Kuhusu kesi ya Lema

Anaandika #Wakili Msomi Peter Kibatala

Tulikubaliana Mawakili wenzangu wa case ya Godbless Lema kuto-post chochote kuhusu case ya Lema mpaka siku Lema anatoka remand; lakini baada ya kuona upotoshwaji na sintofahamu unaofanyika/iliyotokea mitandaoni kuhusu case hii, tumeona ni vyema tukatoa ufafanuzi.

Kama tulivyosema awali; Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha ilimpatia dhamana Lema mnamo tarehe 11 November. Mara baada ya Mahakama kutoa dhamana, Serikali ikatoa taarifa ya kusudio la kukata rufaa dhidi ya uamuzi huo. Tafsiri yao ya sheria husika ni kwamba baada ya taarifa hiyo ya kusudio hilo, Mahakama haina mamlaka ya kuendelea kuweka masharti ya dhamana mpaka rufaa ya serikali itakaposikilizwa na kutolewa uamuzi.
Mahakama ikakubaliana na hoja hiyo na kukata kuweka masharti ya dhamana.

Sisi hatukuridhishwa, na tukaandika barua kwa Judge Mfawidhi wa Mahakama Kuu Kanda ya Arusha ili Mahakama Kuu iitishe Majalada ya case husika na kujiridisha na uhalali wa uamuzi huo. Tulikuwa na sababu za kisheria za hatua hiyo, ikiwemo maoni yetu kwamba uamuzi ule ulikuwa ni mdogo (interlocutory) na hauwezi kukatiwa rufaa au kuombewa marejeo. Mahakama Kuu kwa mamlaka yake ya usimamizi wa Mahakama za chini yake ikatuita kuelezea tatizo.

Kwa bahati mbaya serikali ikawasilisha mapingamizi wakisema tulipaswa kukata rufaa badala ya kuomba Mahakama Kuu iingilie kati kwa mamlaka yake ya usimamizi. Sisi tukasisitiza mamlaka ya usimamizi wa Mahakama Kuu ni kubwa kuliko haki ya kukata rufaa.

Mahakama Kuu mnamo 22/11/2016 ikaelekeza tukate rufaa pamoja na kwamba tayari ilishatuita yenyewe.

Iwe iwavyo, tukapeleka Mahakamani notisi ya kusudio la kukata rufaa. Tukapeleka pia hati ya rufaa.

Leo asubuhi wakati tukijiandaa na usikilizwaji wa Rufaa, serikali ikaleta pingamizi kwamba hatujakidhi takwa la kutoa notisi kabla ya rufaa. Pingamizi lazima lisikilizwe kwanza kwa mujibu wa sheria; vyovyote litakavyomriwa na Mahakama.

Mahakama imeelekeza serikali kuwasilisha hoja zake za maandishi mpaka tarehe 30 November saa 2 asubuhi. Sisi tutajibu siku hiyo hiyo saa 6 mchana, serikali itajibu tena saa 9 alasiri ya siku hiyo hiyo ili uamuzi utolewe tarehe 2 December saa 3 asubuhi. Kisha kutegemea na uamuzi, tutasikiliza rufaa yetu.

Kama tulivyosema awali; michakato ya kisheria huwa haina njia ya mkato. Kwa mfano, mtu akileta pingamizi hakuna namna zaidi ya kulisikiliza kabla ya case/ maombi ya msingi.

Bahati mbaya kuna upotoshwaji unaotokana na baadhi kutaofahamu hasa nini kinatokea mahakamani; kwa mfano, taarifa kwamba leo (28/11/2016) ilikuwa Lema apewe dhamana SI SAHIHI. Leo ilikuwa tusikilizwe rufaa yetu ili kama ilikubalika, Mahakama Kuu iamuru Mahakama ya Hakimu Mkazi au yenyewe itoe dhamana kwa Lema.

Kwa hiyo: tutajadili pingamizi la Serikali na kutegemea na maamuzi ya Mahakama Kuu hapo Ijumaa 2/12/2016, tutasikiliza rufaa ya Lema. Mahakama Kuu inajitahidi sana kushughulikia suala hili kwa haraka kama tulivyoomba kwa hati ya uharaka.

Lema yuko imara kwa kuwa, tofauti na baadhi yetu, anafahamu 100% nini kinaendelea. Anafahamu sacrifices tunazozifanya kwa niaba yake ili hatimaye apate dhamana.

Ametuagiza kusimama imara bila kutetereka kwa kuwa ametuchagua sisi tumpiganie.

Monday, November 28, 2016

hawa maprof wetu now days
https://www.facebook.com/100008744220984/videos/1625207681114024/ 

WANAFUNZI IFM WAVULIWA MAJOHO KATIKATI YA MAHAFALI.


Na Jonas Mushi wa gazeti la Mtanzania.

CHUO cha Usimamizi wa Fedha (IFM) kimeanza utekelezaji wa agizo la Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako, kwa kuwazuia wahitimu wa ngazi ya cheti na stashahada kuvaa majoho na kofia wakati wa mahafali yao.

Kitendo hicho kilitokea katika Viwanja vya Karimjee, Dar es Salaam juzi baada ya mratibu wa mahafali ya 42 ya IFM, Dk. Godwin Kaganda, kutangaza utaratibu huo licha ya wahitimu wao kuvaa majoho yao.
Dk.Kaganda alisema utaratibu huo ni kwa mujibu ya miongozo iliyotolewa na Serikali kuhusu uvaaji wa majoho, ambao unataka yavaliwe na wahitimu wa kuanzia ngazi ya shahada na kuendelea.

“Wahitimu wote wa ngazi ya cheti na stashahada hamtovaa majoho wala kofia pamoja na kwamba mlishapewa awali, tunaomba radhi kwa sababu ndiyo miongozo tuliyopewa,” alisema Dk. Kaganda, (kisha wanafunzi hao kuvua majoho hayo kila mmoja kwa muda wake).

Sunday, November 27, 2016



DEATH OF A REVOLUTIONARY

 Fidel Castro : August 13, 1926 – November 25, 2016 : Death of a Revolutionary
I'm sure most are aware of the sad passing of Cuban Revolutionary
Fidel Alejandro Castro Ruz on November 25. He governed Cuba as Prime Minister from 1959 to 1976 and then as President from 1976 to 2008 and under his administration, Cuba became a one-party socialist state; industry and business were nationalized, and state socialist reforms implemented throughout society.

Born in Birán as the son of a wealthy Spanish farmer, Castro adopted leftist anti-imperialist politics while studying law at the University of Havana. After participating in rebellions against right-wing governments in the Dominican Republic and Colombia, his first attempt to overthrow then Cuban President Fulgencio Batista, by launching an attack on the Moncada Barracks in 1953 failed, landing him in Prison.

After a year's imprisonment, he traveled to Mexico where he formed a revolutionary group, the 26th of July Movement, with his brother Raúl Castro and Che Guevara. Returning to Cuba, Castro took a key role in the Cuban Revolution by leading the Movement in a guerrilla war against Batista's forces from the Sierra Maestra. After Batista's overthrow in 1959, Castro assumed military and political power as Cuba's Prime Minister.

The United States opposed Castro's government, and unsuccessfully attempted to remove him by assassination, economic blockade, and counter-revolution, including the Bay of Pigs Invasion of 1961. Countering these threats, Castro formed an alliance with the Soviet Union. In response to U.S. nuclear missiles in Turkey, and perceived U.S. threats against Cuba, Castro allowed the Soviets to place nuclear weapons on Cuba, sparking the Cuban Missile Crisis—a defining incident of the Cold War—in 1962.

His role in the 1962 Cuban Missile Crisis also ensured that his name was recorded in the annals of Human History.

All in all, Castro cast a polarising figure throughout his life, but those of us in the 'Third World' owe him and the people of Cuba an immeasurable debt by virtue of Castro's willingness to lend Military and financial assistance to the African Liberation Movements across the Continent which led to the end of Colonial Rule. For this alone, we will always honour Fidel since he came to our aid in the hour of our greatest need, when no-one else would help our cause.

As a survivor of covert CIA Cold War operations to depose him such as the failed 'Bay of Pigs Invasion', Castro's leadership was marked by an iron-clad resolve. His Patriotism was best exemplified by his spontaneous fiery speeches against the US & its allies. During these speeches, Castro would literally hold Cubans in a trance as he expressed condemnation at what he rightly believed were ceaseless attempts by the US to depose him, and restore the Country to its former Slave status under the Batsista regime.

He also survived over 600 ingenious assassination attempts including one involvling a plan to poison his Cigars. Within Cuba itself, he was also a polarising figure with some believing that his hold on power had lasted too long, whilst remaining a hero to others.
In the end, I believe we can confidently state that whilst Castro certainly had his flaws, he nevertheless lived out his life to its fullest purpose, and that along the way his path coincided with ours.....We are eternally grateful for that.

Check out the links to the tribute articles below from the New York Times and Al Jazeera which clearly reveal the extent to which Castro even in death continues to polarise the World. We've also added the link to the feature we did recently on the Cuban Missile Crisis as well as the failed plots to assassinate him.

We top it off with 2 of the best Castro documentaries I had the pleasure of watching earlier on in the year...One!
#RIPFidel
New York Times Article: http://www.nytimes.com/…/w…/americas/fidel-castro-dies.html…
Al Jazeera Article: http://www.aljazeera.com/…/cuba-leader-fidel-castro-dead-90…
Our Cuban Missile Crisis Piece: https://www.facebook.com/permalink.php?story_fbid=654567434711285&id=269167643251268&substory_index=0

WATUMISHI WALIOSOMA VYUO VIKUU BILA SIFA KUFUKUZWA KAZI.

Baada ya matamko kadhaa kadhaa ya serikali kuhusu Sekta ya Elimu nchini hatimaye leo limeibuka jingine la kutimua watumishi wote wa umma waliojiunga na vyuo vikuu na kutunukiwa "degree" bila kuwa na sifa.
Hayo yameelezwa na Waziri wa Elimu Prof.Joyce Ndalichako wakati akifungua maonesho ya vyuo vya elimu ya juu yaliyoandaliwa na Tume ya Vyuo vikuu nchini (TCU) yanayofanyika viwanja vya Karimjee, jijini Dar. Maonesho hayo yanashirikisha vyuo 61 ambapo 12 kati ya hivyo ni kutoka nje ya nchi.
Katika taarifa yake Ndalichako amesema Wizara yake inawasiliana na idara ya Utumishi ili kuwabaini watumishi wote waliojiunga vyuo vikuu bila sifa na wafukuzwe kazi. "Kama wewe ni mfanyakazi uliyesoma moja ya vyuo vikuu ukafaulu lakini hukuwa na sifa ya kujiunga na chuo kikuu, tutakunyofoa hukohuko kwenye ajira yako" Alisema Ndalichako.

Kufuatia agizo hilo la Ndalichako, watumishi wote waliosoma vyuo vikuu kwa kupitia foundation courses kama Pre Entry/Remidial/Certificates, etc,wataondolewa kazini. Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa ya kusoma degree. Amesema kuwa kama mtu hakupata points za kumuwezesha kujiunga chuo kikuu hata asome foundation course bado hatapata sifa, namna pekee ya kupata sifa ni kurudia mtihani wa kidato cha sita.

Agizo hilo pia litawagusa watumishi waliojiunga na elimu ya juu kwa ufaulu linganishi (equivalent pass) ambapo kwa wale waliotoka diploma na wakasoma degree bila kufikisha GPA iliyowekwa na NACTE watatimuliwa. Pia waliotoka kidato cha sita na kupata nafasi vyuo vikuu moja kwa moja lakini hawakufikisha "cut off points" zilizowekwa na TCU wataondolewa katika ajira zao.
Prof.Ndalichako amesema zoezi hilo litaanza baada ya kumaliza zoezi la uhakiki wa sifa kwa wanafunzi wanaopata mikopo. "Tukimaliza hawa wanaopata mikopo, tutahamia wasiopata mikopo kuona kama wana sifa za kusoma vyuo vikuu, baadae kwa wafanyakazi. Hata kama hukupata mkopo, lakini ulisoma chuo kikuu bila sifa hauko salama" Alisisitiza Ndalichako.

MARUFUKU WALIOSOMA DIPLOMA KUSOMA DEGREE


Waziri wa Elimu na mafunzo ya ufundi Pro.Joyce Ndalichako amepiga marufuku wanafunzi kujiunga na masomo ya Shahada (degree) bila kupita kidato cha sita. Marufuku hiyo itaanza rasmi katika mwaka ujao wa masomo. Prof.Ndalichako emesema mfumo wa elimu huria umechangia kuzalisha wasomi butu kwa kupokea wanafunzi dhaifu kitaaluma.

Ndalichako amesema wanafunzi wanaofeli kidato cha nne na kwenda kusoma certificate na baadae diploma ili wajiunge vyuo vikuu hawataruhusiwa kujiunga na masomo ya shahada (degree) kama hawajarudia (reseat) masomo yao na kupata alama za kwenda kidato cha tano, na wafanye mitihani ya kidato cha sita na kufaulu ndipo wajiunge vyuo vikuu.

Katika utaratibu huo, wanafunzi wa kidato cha nne watakaoruhusiwa kusoma shahada (degree) bila kupita kidato cha 5 na 6 ni wale waliofaulu kidato cha 4 na wakachaguliwa kwenda kusoma diploma katika mambo kama uganga (clinical medicine), ufundi (technical education), kilimo (agriculture) etc. Lakini sharti wawe wamefaulu kidato cha 4na kuchaguliwa kusoma vyuo vya kati.

Lakini wale wanaokosa "credit" za kuendelea form five na kuamua kwenda certificate mwisho wao utakuwa diploma, na diploma zao hazitaruhusiwa kutumika kama equivalent pass ya kujiunga chuo kukuu hadi watakaporeseat. Diploma watakaoruhusiwa kusoma degree ni waliopita form six, au waliofika form four wakafaulu na kuchaguliwa kwenda vyuo vya kati.

Kuhusu "foundation courses" kwa wanafunzi wa kidato cha sita walioshindwa kupata sifa za kusoma degree, Ndalichako amesema Foundation course haimuongezei mtu sifa. "Kama mtu amemaliza kidato cha 6 akashindwa kufikisha "points" za kujiunga chuo kikuu, asidahiliwe kwa kusoma foundatiom course. Anapaswa kurudia mtihani wa kidato cha 6 kwa sababu baraza la mitihani linatoa fursa ya kurudia mara nyingi iwezekanavyo. Foundation course haimuongezei mtu sifa kama hana sifa zinazotakiwa kitaaluma" Amesisitiza Ndalichako
 

Saturday, November 26, 2016

KATUNIKA

 



Watu 80 wauawa kwenye mlipuko wa kujitoa muhanga nchini Iraq


Shambulizi la kujitoa muhanga kwa mlipuko wa lori la mafuta lililotegwa mabomu lilitokea jana katika kituo cha mafuta mkoani Babil nchini Iraq, na kusababisha vifo vya mahujaji 80 wa Shia na wengine 31 kujeruhiwa.
Shambulizi lilitokea wakati mahujaji hao wakirudi nyumbani kwa mabasi kutoka mji wa Karbala baada ya shughuli ya kidini. Wengi wa waliouawa ni wairan na wapakistani. Kundi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.

Serikali za Iran na Iraq zimelaani vikali shambulizi hilo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Bw. Bahram Qasema amesema kitendo hicho kikatili cha IS ni cha kulipiza kisasi, kutokana na kuendelea kushindwa kwa mfululizo katika mapambano.
KARIBU DAR ES SALAAM aka DSM



R.I.P FIDEL CASTRO


R.I.P FIDEL CASTRO

Rais wa zamani wa Cuba na kiongozi wa chama cha Kikomunisti Fidel Castro Ruz amefariki dunia akiwa na miaka 90.

Kupitia runinga Rais wa sasa wa nchi hiyo ambaye pia ni mdogo wake Raul Castro Ruz amethibitisha kifo cha kaka yake.

The late Fidel Castro Ruz

MATUMIZI YA SADAKA ZENU

Wachungaji Uchwara! Takribani magazeti yote ya leo Yameamka na Lusekelo " Mzee wa Upako" juu ya kukamatwa na jeshi la polisi. Hiki ni kituko alichokifanya na kupelekea kukamatwa kwake. Aliziba njia kwa kupaki gari barabarani na kuwatolea maneno machafu majirani( ulevi noma)
https://www.facebook.com/100008744220984/videos/1623749974593128/

Wednesday, November 23, 2016


THE DEADLIEST SNAKE ON THE PLANET!

Anaitwa Mamba mweusi wa Africa
The African Black Mamba!
Anapatikana katika Bara la Africa tuu...
Ndie nyoka hatari kabisa! Anatoa sumu aina mbili na zote ni noooma! Anatoa sumu inayojulikana kama "Neurotoxin hii huathiri mfumo wa neva
Napia anatoa sumu nyingine aina ya Cardiotoxin hii hushambulia mfumo wa moyo.... Nyoka huyu akikuuma unaweza kufa ndani ya dakika 20!

Black Mamba ninyoka mkorofi katili anasumu kali, anasifa ya urefu kama uavyomuona anafika hadi miguu 14 kwa hesabu za kiswahili! Ye huwa hana mwili mkubwa kama kina Python(Chatu) Mungu ni fundi sana huwa hakosei! Huyu nyoka ana roho mbaya sana kwanza amejaaliwa mbio kuliko nyoka wote! Ukikutana nae kuna ishara kuu mbili atakuonyesha kuwa Mimi African Black Mamba...Nyoka niliye jaaliwa sumu kuliko nyoka wote! 
Ulaya hayupo huyu lakini Wazungu wanamtambua vema wakotaka kuja Afrika kuna viumbe kwanza wanaambiwa mkifika huko mnapaswa kuchukua tahadhari ya hali ya juu na viumbe hivi hatari.. Ktk list huyu nae yumo! So ukipata bahati yakukutana nae kwanza atakutisha! Ata achama kinywa ama mdomo wake wenye rangi nyeusi kwa ndani! Kinywa chake ni cheusi kwa ndani na ndio kimefanya aitwe Black Mamba!
 Pili utamskia anatoa sauiti kama msela anaita demu! Au kama tairi linalotoa upepo...Tatu utamuona anatanua shingo yake japo sio kama ya Cobra!!! Hapo ujue uko mbele ya nyoka hatari kabisa! Uzidishe maombi! Vitu viwili usijethubutu kuvifanya! Moja... Uskimbie.. Maana huyu nyoka anambio zaidi ya Husein Bolt!
 Mamba anakimbia Maili 12 kwa saa... Na akikukimbiza hakubali hadi akugonge sehemu ya mwili wako.. Ye ardhini huwa anateleza! Na ukimkimbia ni lazima tuu atakuunganishia! Na hatakukosa! Pili kuna wale watu akiona tu nyoka ye anakimbilia fimbo au jiwe... Siku ukutana na nyoka huyu jua umekwisha! Wataalam wanakwambia nyoka huyu hapigwi! Kwani hata hilo jiwe huenda usiwahi kulirusha au mfe wote!
 Black Mamba anasifika kwa Show za kikatili anashambulia vibaya sana! Ndio maana nilisema Mungu ni fundi! 
Pamoja na kumuumba nyoka huyu na Sumu kali mbio nyingi, hasira na urefu lakini nyoka huyu amejaaliwa huruma ndani yake ukikutana nae akianza kukuonyesha sarakasi zake kuwa mimi ndie nyoka hatari nawe Binaadam ukijishusha usikimbie wala ustupe jiwe ubaki unamuangalia tuu macho kwa macho! Unaambiwa atatuliza mzuka! Na wala hatakugusa ataingia zake mitini! 
"Unaona Muumba alivyo wa ajabu"!! 
Mamba anataga mayai kama kuku tuu kiota chake huwa ardhini...Jike anataga mayai 10-25 akishataga mayai yake huwa yanajiengua yenyewe baada ya miezi mitatu.
Joto ni muhimu kwaajili ya lncubation...na vitoto vyake vikisha jitotoa unaambiwa vinaanza mishe saa hiyohiyo hujitegemea kwa kilakitu! watoto wake wana sumu kali kama Mama yao yaani haina kuremba!!!
Nyoka huyu anaishi hadi miaka 11 porini... Akiwa anafugwa anaeza ishi hadi miaka 12...... 
 

Friday, November 18, 2016

Rais asaini maswada wa habari, dear Journalist get ready for whatever


MZEE WASIRA AKIKOKOTWA KUTOKA MAHAKAMANI LEO BAADA YA MH TUNDU LISSU , KUMPIGA MAKONDE MAZITO YA VIFUNGU VYA SHERIA WASIRA ALIJIKUTA ANAOMBA MKEKA ILI APUMZIKE KWANI LISSU ALIMALIZA NGUVU KABISA..

BULAYA AMGALAGAZA VIBAYA MZEE WASIRA


MBUNGE WA BUNDA ESTER BULAYA AKIPONGEZANA NA MWANASHERIA ANAEJUA SHERIA KULIKO WANASHERIA WOTE TANZANIA AMBAE PIA NI MWANASHERIA WA CHADEMA MH TUNDU LISSU BAADA YA KUMGALAGAZA VIBAYA MZEE WASIRA..

Ester Bulaya akimpongeza mwanasheria wake Mh. Tundu Lissu baada ya kushinda kesi ya kupinga ushindi wake wa Ubunge iliyofuliwa na wanachama wa CCmM dhidi ya wasira


picha ya katikati na chini wafuasi wa Bulaya wakishangilia ushindi

JPM AANGUSHWA TUZO ZA FORBES (POY) 2016.

JPM AANGUSHWA TUZO ZA FORBES (POY) 2016.


By Malisa GJ,

Rais John Pombe Magufuli ameangushwa katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za Forbes Person of the Year 2016. Mshindi wa tuzo hizo aliyetangazwa usiku huu ni Bi.Thuli Madonsela, Mkurugenzi wa zamani wa mashtaka nchini Afrika Kusini. Katika tuzo hizo zilizokua na washindani watano, Thuli amewashinda marais wawili wa Afrika ambao ni Rais Magufuli na Rais Ameenah Gurib wa Mauritania.

Thuli ambaye kitaaluma ni mwanasheria anasifika kwa ujasiri wake wa kupambana na makosa mbalimbali hasa rushwa baina ya viongozi na watumishi wa umma. Aliteuliwa na Rais Jacob Zuma mwaka 2009 kuwa Mkurugenzi wa mashtaka nchini humo, nafasi aliyoitumikia hadi October 14 mwaka huu.

Miongoni mwa mambo yaliyompatia umaarufu Thuli ni pamoja na kuibua tuhuma mbalimbali zenye "public interest" ikiwemo skendo ya familia ya Gupta ya kuhonga serikali ili kujipatia nafasi za kisiasa na familia hiyo kumshinikiza Rais Zuma kuteua mawaziri wanaowataka. Kashfa hiyo ni maarufu kama "State of Capture"

Pia Thuli alisimama kidete kuhakikisha Rais Zuma anarudisha kiasi cha dola milioni 16 (takribani bilioni 35 za kitanzania) alizotumia kujenga jumba lake la kifahari huko KwaZulu-Natal. Kashfa hii inajulikana kama "Nkandla scandal"
 
 Thuli ni mama wa watoto wawili (wa kike aitwae Wenzile, na wa kiume aitwaye Mbusowabantu), ambao amewalea peke yake (single parenting) tangu mwaka 1980 mumewe alipofariki na kumuachia watoto hao wakiwa wadogo, huku yeue akiwa mama wa miaka 18 tu. Tangu wakati huo Thuli ameishi mjane kwa kipindi chote cha maisha yake akiwalea watoto hao peke yake.

Thuli Madonsela alizaliwa huko Mbabane Swazilaand mwaka 1962 na kuhitimu masomo yake ya sekondari katika shule ya Evelyn Baring High School. Baada ya kuhitimu alibakia shuleni hapo akiwa kama mwalimu msaidizi (Assistant teacher) na mwaka 1982 alihamia nchini Afrika kusini katika mji wa "makabwela" wa Soweto kutafuta maisha, ambapo aliajiriwa katika shule ya Naledi High School kama Mwalimu Msaidizi.

Baadae alirudi nchini Swaziland kujiendeleza kimasomo ambapo alihitimu shahada yake ya kwanza ya sheria (LLB) kutoka chuo kikuu cha Swaziland mwaka 1987, na kisha shahada ya uzamili ya Sheria (LLM) kutoka chuo kikuu cha Witwatersrand mwaka 1990. Thuli amewahi pia kutunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa sheria LLD (Honoris causa) kutoka chuo kikuu cha Stellenbosch, na chuo kikuu cha Cape Town.
Thuli ana umri wa miaka 54, na alikuwa mwanachama wa chama tawala cha ANC hadi mwaka 2007 alipoamua kujiondoa kwenye siasa za vyama.

Wednesday, November 16, 2016

STEND YA MSAMVU MKOANI MOROGORO

stand ya kimataifa ya msamvu iliyopo mkoani morogoro imefuguliwa rasi



Add caption