JPM AANGUSHWA TUZO ZA FORBES (POY) 2016.
By Malisa GJ,
Rais John Pombe Magufuli ameangushwa katika kinyang'anyiro cha kuwania tuzo za Forbes Person of the Year 2016. Mshindi wa tuzo hizo aliyetangazwa usiku huu ni Bi.Thuli Madonsela, Mkurugenzi wa zamani wa mashtaka nchini Afrika Kusini. Katika tuzo hizo zilizokua na washindani watano, Thuli amewashinda marais wawili wa Afrika ambao ni Rais Magufuli na Rais Ameenah Gurib wa Mauritania.
Thuli ambaye kitaaluma ni mwanasheria anasifika kwa ujasiri wake wa kupambana na makosa mbalimbali hasa rushwa baina ya viongozi na watumishi wa umma. Aliteuliwa na Rais Jacob Zuma mwaka 2009 kuwa Mkurugenzi wa mashtaka nchini humo, nafasi aliyoitumikia hadi October 14 mwaka huu.
Miongoni mwa mambo yaliyompatia umaarufu Thuli ni pamoja na kuibua tuhuma mbalimbali zenye "public interest" ikiwemo skendo ya familia ya Gupta ya kuhonga serikali ili kujipatia nafasi za kisiasa na familia hiyo kumshinikiza Rais Zuma kuteua mawaziri wanaowataka. Kashfa hiyo ni maarufu kama "State of Capture"
Pia Thuli alisimama kidete kuhakikisha Rais Zuma anarudisha kiasi cha dola milioni 16 (takribani bilioni 35 za kitanzania) alizotumia kujenga jumba lake la kifahari huko KwaZulu-Natal. Kashfa hii inajulikana kama "Nkandla scandal"
Thuli ni mama wa watoto wawili (wa kike aitwae Wenzile, na wa kiume aitwaye Mbusowabantu), ambao amewalea peke yake (single parenting) tangu mwaka 1980 mumewe alipofariki na kumuachia watoto hao wakiwa wadogo, huku yeue akiwa mama wa miaka 18 tu. Tangu wakati huo Thuli ameishi mjane kwa kipindi chote cha maisha yake akiwalea watoto hao peke yake.
Thuli Madonsela alizaliwa huko Mbabane Swazilaand mwaka 1962 na kuhitimu masomo yake ya sekondari katika shule ya Evelyn Baring High School. Baada ya kuhitimu alibakia shuleni hapo akiwa kama mwalimu msaidizi (Assistant teacher) na mwaka 1982 alihamia nchini Afrika kusini katika mji wa "makabwela" wa Soweto kutafuta maisha, ambapo aliajiriwa katika shule ya Naledi High School kama Mwalimu Msaidizi.
Baadae alirudi nchini Swaziland kujiendeleza kimasomo ambapo alihitimu shahada yake ya kwanza ya sheria (LLB) kutoka chuo kikuu cha Swaziland mwaka 1987, na kisha shahada ya uzamili ya Sheria (LLM) kutoka chuo kikuu cha Witwatersrand mwaka 1990. Thuli amewahi pia kutunukiwa Shahada ya heshima ya udaktari wa sheria LLD (Honoris causa) kutoka chuo kikuu cha Stellenbosch, na chuo kikuu cha Cape Town.
Thuli ana umri wa miaka 54, na alikuwa mwanachama wa chama tawala cha ANC hadi mwaka 2007 alipoamua kujiondoa kwenye siasa za vyama.

No comments:
Post a Comment