Friday, November 11, 2016

KESI YA LEMA YAZIDI KUSHIKA KASI


Hakimu amekataa hoja dhaifu za upande wa Jamhuri za kumnyima Lema dhamana.
Hakimu: sheria ya jinai kifungu 148(c) mshtakiwa atanyimwa dhamana kama angekiuka masharti ya dhamana au kukimbia. Na kuna vifungu vya lazima kwamba mshtakiwa anapaswa kusurender passport au hati za kusafiria au Mahakama ikarestrict maeneo ya kutembelea mfano eneo la kijiji n.k
Jamhuri: Mheshimiwa Hakimu mikutano ya kisiasa hairuhusiwi kwa sasa lakini Lema alifanya.
Hakimu: Mahakama hii wala mahakama ya juu yake haikutoa masharti kuwa mshtakiwa asifanye kosa wala hakuzuiliwa kufanya Mikutano ya hadhara.
Jamhuri: Mheshimiwa Hakimu Lema anapaswa kunyinwa dhamana mwa usalama wa Rais na usalama wake pia?
Hakimu: Kwamba mshtakiwa asipewe dhamana kwa usalama wake what are the tests?? Sio tu kusema ni kwa usalama wake sheria inataka useme kwa hakika kuwa ni lazima. Na hiyo test sio hoja yangu ni test ya High Court ref case ya Athuman Mahumba V/S Jamhuri.
(Mawakili wa Jamhuri wanaangaliana).!
#BinamuBananga
#MahakamaniArusha.!

Mh. Godbless Lema akiwa kwenye harakati za kisiasa

No comments:

Post a Comment