kama anavyoripoti Ally Bananga.
Naibu Katibu Mkuu wa Chadema, Salum Mwalimu amezuiwa kuingia mahakamani. Meya wa jiji la Arusha Kalisti Lazaro nae pia amezuiwa kuingia Mahakamani licha ya kuwa kwenye gari ya serikali. Lakini baada ya kelele za makamanda waliokua Mahakamani hapo hatimaye Mstahiki Meya ameruhusiwa kuingia.
Wakili wa serikali anasema Lema asipewe dhamana kwa kuwa alisema Rais atakufa kwa hiyo akitoka ataweza kuufanikisha mpango huo. Lakini pia anasema mke wa Rais ni mgonjwa kwa sasa na inawezekana ndio sehemu ya maono ya Lema kuidhuru familia ya Rais. Ameongeza kuwa Lema akiachiwa ataendeleza uchochezi na kwamba kubaki kwake ndani ni kwa usalama wa kwake na taifa.
Kesi inaendelea kusikilizwa na Hakimu Kamugisha, na inategemewa haki itatendeka na Lema kupewa dhamana. Tuendelee kusubiri.!
#BinamuBananga
#MahakamaniArusha.!
#BinamuBananga
#MahakamaniArusha.!
![]() |
baadhi ya viongozi wa CADEMA wakiwa nje ya Mahakama ya Arusha baada ya kuzuiwa kuingia |
No comments:
Post a Comment