Wednesday, November 30, 2016

MSIBA MZITO KATIKA MPIRA WA MIGUU DUNIANI

ForçaChapecoense

Uongozi wa Naipenda YANGA unajumuika na wapenda mpira wa miguu duniani kote kutoa simanzi zetu pamoja na mkono wa pole kwa klabu ya Associação Chapecoense de Futebol ya nchini Brazil ambayo imepoteza viongozi wa klabu, benchi zima la ufundi na wachezaji wote 22 (wamepona wawili tu, ambao wako Hospital) waliopata ajali ya ndege nchini Colombia.


*** HISTORIA FUPI YA CHAPECOENSE ***

Ikiwa imeanzishwa mwaka 1973, ilishiriki mara ya kwanza Ligi Kuu ya Brazil, maarufu kama Serie A mwaka 2014, ikiwa imepanda daraja mfululizo kuanzia Serie D mwaka 2009.

Mwaka huu ilifanikiwa kupata uwakilishi kucheza michuano ya Copa Sudamericana (sawa na CAF Confederation Cup ya Afrika au UEFA Europa League ya Ulaya) na ikafanikiwa kutinga fainali kwa mara ya kwanza katika historia yao.

Ikiwa njiani kuelekea nchini Colombia kucheza mechi ya kwanza ya fainali dhidi ya Atletico Nacional ya huko , ndege iliyowabeba yao ilipata ajali kutokana na hitilafu ya umeme na kuanguka karibu na mji wa Medellin, Colombia.

*** MSAADA KWA CHAPECOENSE ***

Klabu zote kubwa nchini Brazil, zimetoa mapendekezo yao kwa Shilikisho la Soka nchini Brazil ikiwa ni jitihada zao kuisaidia timu ya Chapecoense kujijenga upya wakati huu ambapo hawana wachezaji karibu wote, pamoja na benchi zima la ufundi.
Klabu hizo ambazo ni Corinthians, Santos, Sao Paulo na mabingwa wapya Palmeiras, wamewasilisha mapendekezo yafuatayo . . . .
1. Kuipa kinga maalum timu hiyo isishuke daraja kwa misimu mitatu mfululizo kuanzia sasa mpaka itakapojijenga tena upya

2. Kuruhusu klabu yoyote kutoa wachezaji BURE kabisa kwa msimu ujao wa 2017 ili waweze kucheza mechi zao kwa ushindani
- Klabu hizo zimesema zipo tayari kutoa wachezaji wake muhimu wakachezee Chape.

Klabu ya Atletico Nacional ambayo ilikuwa icheze nayo fainali, imeiomba shirikisho la soka la Amerika ya Kusini kuitangaza Chapecoense kama Mabingwa wapya wa Copa Sudamericana 2016, kwa heshima yao kipindi hiki kigumu kwao.

Klabu ya PSG ya Ufaransa tayari imetangaza kutoa Pauni Milioni 40 kusaidia kuijenga upya kikosi cha Chapecoense.


picha zote tatu ni mabaki ya ndege iliyopataajali na kuuwa zaidi ya watu 72
 

No comments:

Post a Comment