Sasa hivi kama unatoka Posta kwenda Mbezi
hakuna daladala zaidi ya Mabasi yaendayo kasi. Utakwenda nayo ukifika
Kimara safari inaisha, unapanda daladala za kawaida kutoka Kimara kwenda
Mbezi.
Nasikia serikali imefanya hivi ili kuondoa ushindani kwa mabasi
yaendayo kasi. Yani waachiwe wenyewe wadominate njia maana walianza
kupoteza wateja na hivyo kujiendesha kwa hasara.
Kama ni kweli
hii si haki kabisa kwa walalahoi ambao usafiri wao mkubwa ni daladala.
Wale wenye magari binafsi watapata ahueni kwa kupunguziwa foleni ya
daladala, lakini walalahoi wataumia sana.
Kwa mfano mlalahoi wa Mbezi alikua akitaka kwenda Kariakoo anapanda
gari moja (TZS 400/=). Lakini sasa hivi atalazimika kupanda magari
mawili. Atapanda Mbezi Kimara 400/= kisha atapanda mwendokasi Kimara
Kariakoo 650/=. So badala ya kufika Kariakoo kwa 500/= kama zamani,
saivi atafika kwa 1,050/=. Ongezeko la 650/=.
Ngoja nikupe mfano
wa pili. Mlalahoi wa Mbezi ambaye ndugu yake amelazwa Muhimbili alikua
anapanda gari moja tu kwa 400/= hadi Muhimbili kwenda kumuuguza ndugu
yake. Lakini kwa utaratibu mpya wa sasa atalazimika kupanda gari 3. Moja
la kutoka Mbezi Kimara 400/=, kisha apande Mwendokasi Kimara Posta
650/= ashuke Fire. Halafu asubirie magari ya Muhimbili yatokayo Buguruni
au Temeke apande kwa 400/=. Jumla 1,450/=. Ongezeko la 1,050/=.
Gharama hizi za nauli zinapanda wakati hali ya uchumi ikizidi kudorora.
Yani mtu aliyekua anaenda Muhimbili kwa TZS 400/= sasa hivi anakwenda
kwa TZS 1,450/=. Wakati huo anamuuguza ndugu yake, na yupo mtaani mwaka
wa pili hana ajira maana serikali imezuia kuajiri kwa muda.
Nadhani serikali ina haja ya kutizama upya jambo hili. Kazi ya serikali
ni kuboresha maisha ya wananchi, na sio kuyafanya yazidi kuwa magumu.!
kitu cha muhimu ni kuboresha huduma na sio kuwamasikinisha wengine
ReplyDelete