Watu 80 wauawa kwenye mlipuko wa kujitoa muhanga nchini Iraq
Shambulizi la kujitoa muhanga kwa mlipuko wa lori la mafuta lililotegwa mabomu lilitokea jana katika kituo cha mafuta mkoani Babil nchini Iraq, na kusababisha vifo vya mahujaji 80 wa Shia na wengine 31 kujeruhiwa.
Shambulizi lilitokea wakati mahujaji hao wakirudi nyumbani kwa mabasi kutoka mji wa Karbala baada ya shughuli ya kidini. Wengi wa waliouawa ni wairan na wapakistani. Kundi la IS limetangaza kuhusika na shambulizi hilo.
Serikali za Iran na Iraq zimelaani vikali shambulizi hilo. Msemaji wa wizara ya mambo ya nje wa Iran Bw. Bahram Qasema amesema kitendo hicho kikatili cha IS ni cha kulipiza kisasi, kutokana na kuendelea kushindwa kwa mfululizo katika mapambano.
No comments:
Post a Comment