"Tumeona Serikali ikivishambulia Vyama
vya Siasa (Kwa kufungia mikutano ya hadhara na wakati fulani hata vikao
vya ndani). Imezishambulia Asasi za Kiraia (Kwa kutishia kuzifutia
usajili Asasi kadhaa, kuwasumbua na kuwatia nguvuni wanaharakati wa haki
za wafugaji huko Loliondo nk).
Sasa wanajiandaa kuvishambulia
vyombo vya habari (Kupitia Muswada wa Sheria ya Huduma za Habari,2016) -
ambao sasa umepitishwa kuwa sheria na bunge. (Tujiulize) ni lini Serikali itaanza kuwashambulia watu wake wenyewe?
Ushambuliaji huu utasababisha hofu na kuzalisha kizazi cha viongozi
ambao hawapokei changamoto ya kukosolewa. Hali hii ni hatari kwa uhai wa
Taifa. Ninainukuu Tahariri ya gazeti la Daily News ya Mwaka 1976 ambayo
ilibatizwa jina la "Tahariri Bora ya Mwaka" wakati huo:
"Yapo
matokeo mawili ambayo ni zao la kukosekana ukosoaji na kujikosoa. Mosi,
kukosolewa na kujikosoa kunapokosekana kwa muda mrefu, viongozi hujikita
katika kupongezana kulikopitiliza na kuanza kuvimba kichwa. Pili,
kukosekana kwa ukosoaji na kujikosoa huzalisha uongozi wa mabavu na usio
na uvumilivu. Viongozi ambao hujiona hawapaswi kuguswa huanza kujihisi
'Miungu Watu'. Bila shaka, haikuwa ajabu Mwaka huo (1976) ndipo Sheria
mbovu ya Magazeti ilipopitishwa"
Sehemu ya Makala ya Ndugu Zitto
Kabwe, Kiongozi wa ACT Wazalendo (Magufuli One Year On: a Shift From
"What Would Magufuli Do" to "What Does Magufuli Want?").
Makala
husika ilichapishwa katika gazeti la the Citizen la tarehe 04 Novemba
2016. Tarjumi/Tafsiri ya makaa hii (Katika lugha ya Kiswahili) imefanywa
na Ndugu Ado Shaibu, Mwenezi ACT Wazalendo (0653619906).
Kuhusu Muswada (Sheria sasa) wa Huduma za Habari, nimeandika. Nimezungumza. Nimetahadharisha.
No comments:
Post a Comment