'Tafuna pesa zao Bastian'
Bastian Schweinsteiger ameambiwa kwamba awaadhibu Manchester United kwa kuutumikia mkataba wake mpaka mwisho wa siku yake.Kiungo huyo mshindi wa kombe la Dunia amekuwa kwenye wakati mgumu kwenye kikosi cha Jose Mourinho mpaka kushindwa kujumuishwa kwenye kikosi cha ligi ya Europa.
Hivi karibu Mourinho alimjumuisha Bastian kwenye kikosi cha kwanza Man United lakini bado hajacheza hata mechi moja kuelekea miezi yake 18 ya mwisho wa mkataba wake.
Sasa, Rais wake wa zamani katika klabu ya Bayern Munich Uli Hoeness amemshauri kwamba achukue kila salio la pesa kutoka Man United kabla ya kuachana na soka .
"kama ningekuwa mimi,ningewakomesha watu wa Manchester wanilipe mpaka mwisho wa mkataba wangu"
"Hicho ndio klabu kama hii inastahili kufanyiwa kwa kile wanachomfanyia. Lazima waadhibiwe."
Mapema mwaka huu Schweinsteiger alisema kwamba Manchester United itakuwa klabu yake ya mwisho barani Ulaya na kuibua tetesi kwamba huenda akahamia Major League Soccer. Lakini Hoeness alisema," kwa nilichokisikia, Basti anaelekea kuachana na soka, namjua vizuri sana nina mashaka sana kama bado ana moto wa kukabiliana na changamoto nyingine tena
No comments:
Post a Comment