Friday, November 11, 2016

OPERESHENI ZA KIJESHI ZAPTEZA MAKAZI 45,000 IRAQ




Watu 45,000 wapoteza makazi kutokana na operesheni za kijeshi kaskazini mwa Iraq

Ofisi ya uratibu wa mambo ya kibinadamu ya Umoja wa Mataifa OCHA imesema watu 3,300 wamepoteza makazi yao kuanzia Jumatano, na kuifanya jumla ya watu waliopoteza makazi tangu mwezi Oktoba operesheni za kijeshi zilipoanza mjini Mosul izidi elfu 45.

Msemaji wa Umoja wa Mataifa Bw. Stephane Dujarric amesema kwa idadi hiyo, kambi zilizopo zinatosha kwa sasa, lakini katika wiki zijazo inahitaji maeneo zaidi ya kujenga kambi na makazi ya dharura, ili kupokea wakimbizi zaidi wa ndani.

wananchi wa Iraq wakikimbia mapigano yanayoendelea Kaskazini mwa nchi hiyo

No comments:

Post a Comment