kwa hisani ya UKUTA Arusha
Jeshi la Polisi mkoani Arusha limepewa nusu saa (dakika 30) kuhakikisha
limemfikisha Mbunge wa Arusha mjini Mhe.Godbless Lema Mahakamani. Amri
hiyo imetolewa na Mahakama kuu mkoani humo kufuatia shauri
lililofunguliwa na Mwanasheria wa Chadema, Wakili (msomi) Jonh Mallya
aliyeiomba Mahakama hiyo kutoa amri ya kachiwa Lema kutoka mikononi mwa
polisi ambapo anashikiliwa kwa muda wa
siku 5 bila kupelekwa Mahakamani. Katika shauri hilo Mallya alisema
Polisi wanamshikilia Lema kinyume cha sheria kwa muda wa siku 5 kwa
madai kuwa mahojiano hayajakamilika. Mahakama kuu imekubaliana na hoja
za Mallya na kuamuru Polisi kumfikisha Lema mahakamani hapo ndani ya
nusu saa kuanzia sasa.
No comments:
Post a Comment