Friday, November 11, 2016

ALEPPO YAKABILIWA NA UPUNGUFU WA CHAKULA NCHINI SYRIA



Sehemu za mashariki mwa Aleppo zakabiliwa na upungufu wa chakula

Mshauri maalumu wa Umoja wa Mataifa kuhusu masuala ya Syria Bw. Jan Egeland amesema majira ya baridi ya mwaka huu yatakuwa mabaya zaidi kwa Syria ambayo imekuwa kwenye mgogoro kwa miaka 5.
Sehemu za mashariki mwa Aleppo, mji ulioko kaskazini mwa nchi hiyo zinakabiliwa na hatari ya kukosa chakula baada ya chakula kilichopo kusambazwa.

Umoja wa mataifa umetoa mpango wa kuzipatia sehemu hizo msaada wa chakula na dawa. Pia ameongeza kuwa sehemu hiyo bado inagombewa na serikali ya rais Bashar na waasi. Kama pande zinazopambana zikikubali mpango huo, itachukua saa 72 kwa timu ya Umoja wa mataifa kuandaa operesheni za msaada na siku nyingine kadhaa kuzitekeleza.

Tangu mapambano yalipuke mwezi wa Machi mwaka 2011, hali katika sehemu mbalimbali za Syria zilizokumbwa na mapambano ni ya wasiwasi mkubwa. Katika mapigano ya miaka 5, watu zaidi ya laki 4 wamefariki na wengine wengi kuwa wakimbizi.

baadhi ya Majengo yakiwa yameharibiwa vibaya Mashariki mwa Aleppo nchini Syria

No comments:

Post a Comment